Habari hizi wakuu ziko confirmed (matokeo ya awali Pending to be announced by ZEC) niko Pemba na ndio narudi kujipumzisha baada ya kuzungukia maeneo yote na kukusanya matokeo. Kwa upande wa Unguja, mpaka sasa CUF wameshinda Jimbo la Mji Mkongwe Uwakilishi(confirmed) pia kuna habari za kwamba wameshinda jimbo la Magogoni (Uwakilishi) na jimbo la Mtoni kwa Maalim Seif. Hata hivyo Mpaka sasa Mawakala wa CCM katika majimbo hayo mawili wamekataa kusign matokeo. Kuhusu ubunge mtakumbuka jimbo la Mji Mkongwe na Magogoni uchaguzi umehairishwa kwa kutofika vifaa vya kupigia kura, wakati Jimbo la mtoni sina habari za uhakika nani kashinda ubunge