CUF Yamaliza Rasmi Kususia Uandikishaji: Watu kuandikishwa bila ZID.

CUF Yamaliza Rasmi Kususia Uandikishaji: Watu kuandikishwa bila ZID.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Chama cha Wananchi, CUF, kimemaliza rasmi ule msuso wa kujiandikisha kwenye maboresho ya daftari la kudumu la kupiga kura, baada ya kuwahimiza wafuasi wake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari hilo.

Taarifa ya CUF kwa vyombo vya habari, pia imewataka wale wote walipiga kura mwaka 2005, ambao bado wanazo shahada zao, wajitokeze kuandikishwa bila kuhitajika kuwa na vitambulisho vya ukaazi. Kwa maneno mengine lile shuruti la kitambulisho cha ukaazi, limeondolewa kwa waliopiga kura mwaka 2005.

Sijui kwanini taarifa hii imetolewa na CUF ilhali ilitakiwa kutolewa na ZEK.
Taatifa yenyewe ni hii hapa
 

Attachments

kwani issue ya sharti la vitambulisho la ukaazi si ilikuwa mbinu tu ya CCM kuvuruga kazi hiyo ya uandikishaji.
 
Natumai mambo sasa yatakuwa mazuri labda kidudu mtu aingie kati kutibua mambo...
 
Naona ni matokeo ya kikao cha dharura cha baraza la mapinduzi lakini ni inshara njema kwa ajili ya uchaguzi wa haki
 
Back
Top Bottom