CUF yazindua Kongamano la kudai Katiba mpya, yataka maoni ya wananchi kuheshimiwa

Wajumbe wa kongamano hilo ni akina nani?

isiwe ni wamachinga wa Buguruni na wachovu wa kariakoo na Manzese?

Ili kongamano liwe CREDIBLE wahudhurie angalau watu wasomi, wanasheria, viongiz wastaafu, vyama vya siasa makini na pengine baadhi ya mabalozia au wawakilishi wao
 
Hongera CUF, ni jukukumu letu sote kama Watanzania kupambania hili kwa umoja na ustawi wa taifa letu. Unafiki una mwisho mbaya.
 
Huyu Mzee kwanza anadaiwa ile hela ya RUZUKU, ile walikuwa wanagawania pale benki ya NMB magomeni wakishirikiana na Msajili wa vyama
 
Huenda Lipumba ni mpinzani wa kweli aliyeamua kumkataa Lowasa asiwe rais kutokana na rekodi zake mbaya huko nyuma na pia huenda Lipumba aliamua kumnyoosha Maalim Seif mtu ambaye sote tumeona ni mbinafsi kupindukia
Kukaa kimya ni busara pia
 
Unafiki tuu.. Ccm B wanahangaika kuingiza wananchi chaka
 
Hongera CUF, ni jukukumu letu sote kama Watanzania kupambania hili kwa umoja na ustawi wa taifa letu. Unafiki una mwisho mbaya.
Yaani ccm ndo mnadai Katiba mpya na Tume huru? Makubwa🙄
 
Nina wasiwasi na hii kauli isijekuwa anatumika, katiba mpya ikija sasaivi ndio tunaenda kumalizwa kule bungeni wooote ni watu wa Ndioooo....,
 
CUF ina wabunge wangapi kwa sasa? Je na wao wak katika SUK?
 
Mbona yeye hataki kutoka cuf?
Siyo hataki kutoka ila hatoki kwa sababu Katiba ya Chama chake inaruhusu na wanachama wanamtaka aendelee lakini Katiba ya Tanzania, pamoja na ubovu wake, inaruhusu Vipindi viwili tu ikiwa na maana Rais wetu mpendwa ambaye sasa hapendeki kama mwanzo, tayari amefika kipindi cha mwisho. Wasiwasi wa wengi anaweza akabadili Katiba kwa msaada wa Bunge dhaifu linaloongozwa na Spika dhaifu na Wabunge dhaifu wa CCM walioingia kwa Uchafuzi wa mwaka huu.
 
😂😂😂😂kupata vichekesho kama hivi napiga namba gani?
 
This is madness. You request and beg the president to initiate the process to a new constitution? We have to demand it radically. We need a serious new front; a front not under the leadership of coward and controversial individuals who have once betrayed "UKAWA". You very well know the president's stand and particularly the CCM election manifesto that the new constitution is not a priority and not even mentioned.
 
Fahamu kuwa vitendo vya uvunjaji wa katiba ya sasa vinafanywa na wateule wa rais au rais mwenyewe. Hii ni kwasababu katiba ya sasa inamlinda na inampa rais mamlaka yaliyopitiliza kiasi cha kuingilia utendaji wa mihimili mingine ya serikali. Kudai katiba mpya ndo njia pekee ya kukomesha hayo yote.
 


I smell a dead rat in this campaign!

It sounds like a front for something.....

let’s say they complete their campaigns and collect the so called “maoni ya wananchi” only to come back and say “wananchi asilimia 80 wamesema hakuna umuhimu wa katiba mpya na wamemuomba aendelee kuwepo ili akamilishe aliyoyaanzisha”........chapter closed and the real ride starts!
 
Ndiyo maandalizi yako ya kutoa stress zenu.Katiba mpya na kuukuu unamwachia nani.Maoni utayapata wapi!!!!!! Hujui kama ccm ni majority na wanahaki ya kuwasikilizA minority, lakini pia wana nafasi ya kuamua kile chenye maslahi kwa taifa.Wewe unamsikiliza le professeee aliyeibuka na hoja ati namba yake ya karatasi za kupigia kura zilinakiriwa na wasimamizi.Wakati utaratibu huo upo tangu 1995 na yeye kaja kugundua 2020 na kudai ni kinyume.Loooooooo le profeseee majanga makubwa, ati anaongoza harakati za kudai katiba mpya.Mmeliwa tigo wakubwa
 
Ingekuwa inakubalika na wananchi ni kweli haiwezi kufa, hata ikifanyiwa hujuma na dola. Kuna uwezekano isife, lakini isiwe na support na wananchi wengi kama ilivyokuwa awali.
Chadema inakubalika kama awali? Ina tofauti na CUF? Ahahahahah!!
 
Chadema inakubalika kama awali? Ina tofauti na CUF? Ahahahahah!!

Magufuli ndio hataki kuona watu wanaikubali cdm. Bila matumizi mabaya ya madaraka hakuna uwezekano wa kuifanya cdm isiwafikie watu wengi sana. Ndio maana Magufuli yuko radhi hata wananchi wote wafe, kuliko kuona wananchi wanaonyesha hisia zao za kuikubali cdm hadharani. Na atatoka madarakani bila kufanikiwa kuua mapenzi ya wananchi kwa cdm.
 
CUF imefufuka lini tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…