CUF ZNZ wazuiwa kujiandikisha.

Kaitaba

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2009
Posts
915
Reaction score
54
Watu wasiofahamika huko Zanzibar, wameanza kuzuia wanachama wa CUF kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura,

Watu hao wanapita kwenye maeneo ambayo ni ngome za CUF na kutangaza kuwa atakaye toka nje na kwenda kujiandikisha atakipata cha moto.

Nawataharifu washika dau wote katika hili kulishughulikia haraka sana kabla mabaya zaidi hayajatokea
 
Viongozi wao walishamaliza ile "operation zinduka against Chadema?"
Maana badala ya kutumia nguvu zao kuzuia mambo kama haya, wao wanageukia Chadema kana kwamba ndio adui yao
 
Mabomu na risasi vimelindima leo huko Zanzibar, na hatimaye kile kilichodhamiliwa (kuzuia kuandikisha wapiga kura) kimekamilika, maana zoezi hilo limesitishwa leo.

Tutarajie mauaji mengine mwakani,

Wenye familia huku bara ni vyema wakae mkao wa kupokea wakimbizi, dalili sio nzuri.
 
Tabaan . Dunia inabadilika. Angalia hali inavyokwenda Ulimwenguni na zile sehemu ambako makundi ya wanaoshindwa katika kura (uchaguzi) halali yanavyoshughulikiwa pale wanapoleta fujo. na angalia jinsi gani vilio vyao vinavyozingatiwa wakati huu. Usidhani mkilia kama mlivyolia wakati ule -mtasikilizwa kama mlivyosikilizwa wakati ule. La busara wakati huu ni Dola kuimarisha tu vyombo vyake vya ulinzi ili kuweza kukabili chochoko zozote za vitimbakwiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…