GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
Even the king of Jungle (The lion) has an end, it can never hunt again to feed its stomach due to oldness.
Hakuna wakati mgumu Chama cha Mapinduzi kinapita kama wakati huu. Chama kimekosa wanamkakati wa kushawishi na kuuza sera kwa wananchi.
Katibu Mkuu Ndugu Bashiru Ally na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ndugu Humprey Polepole ni moja kati ya makatibu waliofeli na kushindwa ndani ya Chama cha Mapinduzi, wamejawa hofu ya upinzani.
Utamaduni wa uwoga na kuogopa kujibu hoja sasa ndio umejengeka ndani ya Chama cha Mapinduzi. Hakuna katibu kati ya hawa wawili mwenye uwezo wa kujibu hoja au kushiriki mdahalo kwa sasa unaohusu demokrasia au uhuru wa habari.
Kauli ya Rais Mstaafu Kikwete kuwa hoja hujibiwa na hoja zaidi na si kupigwa nyundo, inaakisi hali halisi kwa sasa ndani ya Chama cha Mapinduzi.
Yafuatayo yanapaswa kuangaliwa na kuchukuliwa hatua za haraka kujenga taasisi hii ya Chama cha Mapinduzi kuwa imara.
Mosi, kuwapa nguvu vijana au damu mpya toka vyuo vikuu uwezo wa kuhoji na kufanya mdahalo. Chama hapa kitakuwa na succession plan baada ya mfumo wa hofu kuondoka.
Pili, chama kitafute mbinu mpya za kuuza sera kwa wananchi kwa kukaribisha midahalo toka kwa watu wenye mawazo tofauti hapa ni kushirikisha wanahabari na asasi za kiraia. Hii itawajengea wananchi imani hasa wale wenye mlengo kuwa chama ni cha kizee.
Chama kutowapa nafasi wale wote waliohamia kwa maslahi binafsi toka nje ya mfumo wa chipukizi. Nafasi zikihitajika washindanishwe kwa hoja na uhuru bila mamlaka kuu kumbeba mhamiaji chamani. Hii itajenga uwajibikaji na uamimifu kwa makada waliopo chamani.
Chama kinatakiwa kujenga upya imani kwa wahisani na marafiki zetu wa siku nyingi hasa Benki ya Dunia na IMF kwa kusimamia kikamilifu sera na mikataba tunayoingia. Haya mambo ya kesi za ajabu ajabu zisizokuwa na mkia wala kichwa za uchochezi na Facebook hazina tija kwa Taifa.
Ni muda muafaka wa chama kukemea kauli tata na za utoto toka kwa viongozi vijana ili kujenga umoja. Ni wakati vijana kuelimishwa huu uhuru tuliupata vipi na kina nani walishiriki. Ni muda wa chama kufundisha vijana huu umoja wa Watanzania ulijengwa vipi.
Chama ni muhimu kikaacha kufanya kazi kwa kutumia wachumia tumbo na wapiga matarumbeta kwa ajili ya kulisha familia zao. Ni muda wa kuombana msamaha na kusahihisha kutokuelewana; chama kijikite kujibu hoja za msingi toka kwa wananchi na nchi wahisani.
Ni muda muafaka wa chama kuachana na hofu isiyoonekana toka kwa makundi kinzani bali ni muda wa kukusanya hoja toka kwa makundi mbalimbali na kuyafanyia utafiti. Report za chama zijengwe kwa tafiti na takwimu za ushawishi.
Huawei Nova 6 5G