Cum cruce et gradio: Mfahamu Thomas Aquinnas moja kati ya watu wenye akili nyingi aliyewahi kuwepo

Cum cruce et gradio: Mfahamu Thomas Aquinnas moja kati ya watu wenye akili nyingi aliyewahi kuwepo

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
35,812
Reaction score
107,628
MATE,
Mwaka 33AD baada ya Kristo kuondoka duniani aliliacha kanisa mikononi mwa Peter kama papa/baba wa kwanza katika kueneza Imani na ushuhuda wa Kristo, Paulo akishirikiana na mitume/wanafunzi wateule kumi na moja na wengine wengii ambao hawajaoredheshwa walijitoa kwa kila hali ili kueneza Imani ya Kristo.

Walikumbana tatizo moja la kutokua na watu/wafuasi wasomi wenye kuweza kuchambua hoja za kifalsafa na kisomi pindi walipokua wanakutana na wasomi nguli wa Imani mbalimbali (falisayo,kayafa,na Athiest mbalimbali). Mitume Wengi walikua ni wayahudi wa tabaka la chini kabisa na maskini hivyo walikua wamepata elimu ya msingi/basic tu ya kiyahudi ambayo waliipata kutoka kwa watu ambao walifahamika kama “Rabi”.

Hawa walikua ni walimu wa kiyahudi ambao walikua wanawafundisha watoto/vijana elimu hiyo ya msingi hasa walifundisha torati ya musa, tamaduni na mila za wayahudi pia waliwafundisha kusoma na kuandika – Yesu pia alipata elimu hiyo.

Baadae alitokea Paulo huyu alikua na elimu kubwa tu aliyoipata kwa ufadhili wa dola la kirumi, alikua kapiga shule vilivyo kanisa likaweka rekodi ya kuwa na mtume ambaye ni msomi kisha baadae alijiuga msomi mwingine aliyefahamika kama Luka

Huyu alikua mwanahistaoria,mwanafiziksi na daktari wa bainaadam alitokea Antioki Syria, jamaa alikua shule imemkaa kichwani. Ni moja kati ya watu waliotunukiwa heshima ya Daktari wa kanisa (Doctor of the church), hii ni heshima wanayopewa watu waliofanya mambo makubwa katika kanisa..baadhi yao ni Jerome,Augustiono. Miaka ilizidi kwenda kanisa likazidi kuchanja mbuga na kumea sehemu mbalimbali za dunia kwa kutumia andiko lile la “Enendeni duniani kote mkawafanye matiafa yote kua wanafunzi wangu”kutokana na kusambaa kwa Imani wakatokea wanazuoni mbalimbali walijitokeza kuhoji uhalali na chanzo hasa cha huyo Mungu/Yesu wanayemtangaza…Baadae alitokea mtu aliyekuja kuvunja hoja zote za Athiest wote yeye ndio kachangia sehemu kubwa sana katika kuimarisha Imani ya Kanisa katoliki kua kama hivi ilivyo leo.

Dvo copiosissimi Indices
Mnamo mwaka 1225 familiaya baba Landulf na mama Theodora kutoka kaktika eneo la Roccasecca, Aquinnas walijaliwa kupata motto wa kiume ambae walimwita Thomas, familia yabwana Landulf ilikua ni yenye uwezo maana yeye mwenyewe alikua mtawala wa Knight [mwanajeshi cheo cha juu ] katika utawala wa King Roger II kaka zake wote walikua ni wanajeshi.

Thomas akiwa na miaka alianza shule, baadae mwaka 1239 Thomas alienda chuoni huko ndio akaanza kuvutiwa na maandiko mbalimbali ya wanafalsafa wa zamani Aristotle, Averroes na Maimonides, ambao kutakana na hoja zao waliwea kumvutia na kumuongezea uwezo wa kutafakari na kuchambua mambo,akiwa huko alikutana na mwalimu wake ambae pia alikua ni padre aitwae John, padr huyu alimshawishi Thomas kujiung na shirika la mapadri waDominca [Dominican Order iliundwa na mtakatifu Dominic], sasa swala la yeye kujiunga na shirika la mapadr halikuawapendea wazazi wake hivyo mapadri wa shirika hilo walimtorosha Thomas kwenda Roma ili wazazi wasiingilie chaguo la mwanawe la kua padre.

Akiwa njiani Thomas alikamatwa na kaka zake waliogizwa na mama yake walimkata na kumrudisha nyumbani ambako huko alifungwa mwaka mmoja kifungocha jela ya nyumbani, ili kudhoofisha Imani na misimamo yake kaka zake walienda kumtafutia mwanamke siku moja ila kijana alijikaza hakuweza kushawishika kwa hili usiku wa siku hiyo alitokewa na malaika wawili ndotoni kumtia moyo juu ya iamani yake….baadae mama yake alipanga njia ya kumtorosha mwanae kwa siri ili aende akajiunge na shirika hilo lamapadri. Mama yakealiona kwamba ili kulinda heshima ya famiia yao bora afanye kwamba Thomas alitoroka ila sio kumruhusu aende kujiunga na mapadri.

Kihaiba Thomas alikuani Introvert sio muongeaji sana hadi kipindi alipokua chuoni huko Paris wanafunzi wenzake walikua wanamuona nimtu hopeless na mjinga, ila mwalimu wake aliyetoka nae Itay alikua anawaambia kwamba mnamdharau ila sikumoja mtakuja kumuheshimu kwa mafundisho yake.Dogo aliendelea na shule akipiga Theology huko aliandika maandiko mengi yaliyohusu Imani.
1604961855052.png

Thomas alipohitimu elimu yake ya Theology alitoa maisha yake yote katika kusafiri sehemu mbalimbali na kuhubiri katika hadhara,kufundisha na kuandika mambo mbalimbali. Kipindi hicho sasa kanisa lilikumbwa na wimbi la watu[phylosophers] waliokua wanahoji kuhusu uhalili na uwepo wa Mungu. Walikua wanatafuta uhusiano kati yay a Imani na Falsafa. Hapo ndipo Thomas alipoanza kuonekana uwezo wake aliojaliwa kutokana na hoja mbalimbali alizoweza kujenga kuhusu Mungu

Watu walikuwa wakipingana kuhusu jinsi ya kuunganisha maarifa waliyoyapata kupitia ufunuo na habari walizoziona kwa kawaida wakitumia akili na hisia zao. Kulingana na nadharia ya Averroes yaani ukweli maradufu [double truth], "aina mbili za maarifa zilikuwa zikipingana moja kwa moja. Maoni ya kimapinduzi ya Thomas Aquinas yalikataa nadharia ya Averroes, akisisitiza kwamba "aina zote za maarifa hutoka kwa Mungu" na kwa hivyo zilifanana. Sio tu kwamba zilikuwa zinaendana, kulingana na itikadi ya Thomas, lakini pia zinaweza kufanya kazi kwa kushirikiana: Aliamini kuwa ufunuo unaweza kuongoza mawazo na kuyazuia kufanya makosa, pia mawazo yanaweza kufafanua na kudhibitisha imani

Thomas alithibitisha uwepo wa Mungu kwa kutumia njia tano ambazo ni: 1) kuangalia ulimwenguni unavyozunguka kama uthibitisho wa Mungu, "muhamishaji asiyehama"; 2) kuchunguza sababu na athari na kumtambua Mungu kama sababu ya kila kitu; 3) kuhitimisha kuwa hali ya kutodumu ya viumbe inathibitisha uwepo wa kiumbe wa lazima, Mungu, ambaye mwanadamu anatoka ndani yake tu; 4) kutambua viwango tofauti vya ukamilifu wa mwanadamu na kuamua kuwa kiumbe aliye juu kabisa, mkamilifu lazima awepo; na 5) Kujua kuwa viumbe vya asili havingeweza kuwa na akili bila kupewa akili na Mungu. Baada ya kutetea uwezo wa watu kujua uthibitisho wa Mungu, Thomas pia alifanya kila njia kulinda taswila ya Mungu kwa kujenga hoja na kuthibitisha Mungu ndie mwenye Nguvu na uweza wote.

Thomas aliamini kwamba sheria za dola zilikuwepo, na zilikuwa muhimu kwa ustawi wa jamii. Kwa kufuata sheria za dola, watu wanaweza kupata wokovu wa milele wa nafsi zao katika maisha ya baadaye. Thomas alitambua aina tatu za sheria: sharia ya asili, sharia chanya na sharia ya milele. Kwa mujibu wa maelezo yake, sheria ya asili inamsukuma mwanadamu kutenda kama inavyotakiwa na kufikia malengo yake na kusimamia haki yake ya kujua mema na mabaya; sheria chanya ni sheria ya dolai, au serikali, na inapaswa kuonyeshwa na sheria ya asili; na sheria ya milele, katika kesi ya viumbe vya busara, inategemea mawazo/fikra na imewekwa katika matendo kupitia uwezo wa mwanadamu kuweza kuchagua kutenda mema au mabaya [free will], ambayo pia inafanya kazi ya kutimiza malengo ya kiroho ya mwanadamu.
1604961979192.png

Thomas anatambulika kama moja ya wanadamu walioweza kumweleza na kumtetea Mungu kupitia mafundisho yake, yeye ndio aliyeweza kudadavua ni jinsi gani mwana damu ana Free will katika maisha yake,kaandika vitabu vingi vya Imani yake akieleza uhusiano wa maisha ya mwanadamu na Mungu (Nguvu ya Asili) Moja ya kitabu chake maarufu ambacho kinatumiwa kufundishwa katika vyuo vya kidini katika Theology kinaitwa Summa Theologica ..mawazo na mchango wake katika kanisa ndio umefanya RC kua hivi ilivyo leo kiimani, wenyewe wanamwita The Universal Teacher, March 7 1274 Thomas aliafariki akiwa na umri wa miaka 48 mwaka 1323 akafanywa kuwa mtakatifu. Mafundisho yake yakawa mwanga waaisha ya wanadamu wengi duniani Mtakatifu Thomas Aquinnas

kwenye moja nyuzi zangu nilieleza jinsi gani kwa Mungu muda haupo, binafsi nilijua mimi ndio mtu wa kwanza kuwaza hivyo na nilitoa mawazo yangu..kumbe Thomas nae alikua ashaelezea miaka 800+ iliyopita wakati akilezea existence of God..mawazo yake na yangu yamefanana kwa kiasi kikubwa yeye anasema Muda ni moja ya viumbe wa Mungu.
Katika mwendelezo wa kuwafanya mataifa yote kua wanafunzi wake (Yesu) na kuilinda imaniya kanisa katoliki alitokea bwana mmoja miaka kadhaa baada ya kifo cha Thomas ambae ameifanya RC kua moja ya Taasisi kubwa na Imara Zaidi ulimwenguni katika kila Nyanja

Ad maiorem Dei gloriam
Íñigo López (tamka Inyigo) alizaliwa October 23 mwaka 1491 nchi Hispania katika mji wa Azpeitia ndani ya kijiji kidogo kiitwacho Loyola. Alikua mtoto mdogo kabisa kati ya watoto kumia na tatu. Toka alipokua mdogo alikua anapenda sana kua mwanajeshi hivyo alipofika umri wa miaka 18 tayari alikua kashavaa gwanda rasmi na kua mwanajeshi, kapigana vita nyingi tu bila kuumia ila mwaka 1521 alipigana vita akavunjika mguu wa kulia akarudi nyumbani kutibiwa baada ya kutibiwa ikaonekana mguu uliovunjika ni mfupi hivyo haitawezekana kwenda jeshini.

Wakati anatibia mguu wake yupo nyumbani tu ndipo alipopata wazo la kuokoka kiroho dada yake alikua anamletea vitabu mbalimbalivya dini vilivyohusu maisha ya Yesu na watakatifu. Katika kusoma soma ndipo alipokutana na kitabu hiki cha De Vita Christi (the life of Christ) ambacho ni kitabu kinachoelezea maisha ya yesu,muongozo wa kiroho,maombi na funga mbalimbali.Alitokea kumpenda mtakatifu franscis wa Asizi hivyo akamfanya kua role model wake. Baadae jamaa ilibidi aende shule maana alikua hana elimu kubwa kihivyo kama mnavyojua wanajeshi wetu, upako ulimtembelea sana hadi akawa anapita mtaani anahubiri lakini baadae aliziwiliwa maana ilikua hairuhusiwi kuhubiri kama hauna degree ya Theology.

Alihamia jiji la Paris kusoma mwaka 153 alihitimu Master of Arts degree, kipindi alipokua huko ndipo vuguvugu la kupambana na wazushi [Anti-protestant] lilikua limepamba moto hivyo Ininyo alikusanya kundi la marafiki zake aliokuta shuleni ambao ni Mtakatifu Francis Xaver, Alfonso Salmeron, Diego Laynez, Nicholas Bobadilla,Peter Faber, na Simão Rodrigues hawa majamaa walikua kweli wanatamani kua mapadri ila bahati haikua upande wao kati ya ni mmoja tu ndio alikua padre lakini hawakuvunjika moyo asubuhi ya tarehe 15 August 1534 walikula kiapo wao wenyewe kwa kujiapisha na kujikabidhi kwa Mungu kufanya kazi yake ya kulinda Imani.

Mwaka1539 ininyo akishirikiana na marafiki zake alianzisha sirika la Jesus Society (Jesuist) yeye akiwa kiongozi mkuu, Hapo tayari alikua haitwi tena Ininyo bali Ignatius, Jesuit ililasimishwa na pope paul III mwaka 1540, Ignatus aliwatuma marafiki zake wale kama wamisionari wake kuzunguka bara lote la ulaya..lengo kuu ilikua kujenga shule,vyuona seminari za kikatoliki ulaya yote. Mwaka 1553 Ingantius aliandika katiba ya shirika la Jesuist akisaidiana na secretary wake Alfonso de Polanco alisisitiza kujikana na utii kwa Papa na kwa wakuu katika uongozi wa Kanisa, kwa kutumia kauli mbiu ya perinde ac cadaver yaani “ kama mwili uliokufa/mfu",akimaanisha kwamba mshirika wa kundi la Jesuist anapaswa kuwa na nidhamu kama mtu aliyekufa. Baadae kanuni yake ya Ad maiorem Dei gloriam ("kwa ajili ya utukufu mkuu wa Mungu’) ndio ikawa kauli mbiu kuu ya shirika la jesuist

Santa alleanza
Jesus society walitembea na vitu vitatu imani,elimu na afya. waliamini kwamba ili kanisa lidumu kwanya watu wake wapewe elimu na afya bora kisha wapondwe pondwe mioyo yao kwa imani..kwa kufuata farsafa hiyo JS wamejenga shule,vyuo,seminari na hospitali nyingi sana duniani kote. Ndio maana utakuta parokia inamiliki shule na hospitali au wanakua na maeneo makubwa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali zakijamii.

Mbali na hayo pia Jesuist ipo kama kitengo binafsi ndani ya kanisa ambacho lengo lakekuu ni kuhakikisha Kanisa katoliki kama taasisi na Imani inaendelea kuwepo kwa kulindwa iwe kwa hali yoyote, sasa basi walipowekeya zaidi kwenye elimuhapo ndio walipojipatia point muhimu za mezani. Kupitia elimu inayotolewa kwenye shule na seminari za katoliki wameweza kuana ushawishi wa serikali nyingi hapa duniani maana viongozi wengi wa serikali na watu wengi wenye ushawishi kwenye jamii ni zao la Jesuist, hivyo wanapata nafasi ya kua na sauti kwenye nchi mbalimbali. Nyerere pia ni zao la jesuist ndio maana alipokua raisi tu alilikabidhi taifa chini ya uangalizi wa mama Bikira Maria..japo watu wa upande wapili hawakupenda kitu hicho ndio maana hua wanamuAddress Kama dikteta na kafir.

Ndani ya Jesuist lilianzishwa shirika la Kukusanya na kuchabua taarifa mbalimbali/shirika la kijasusi linaloitwa Santa alleanza (holy alliance) au LeEntita. shirika hili lilianzishwa na Papa Pius V mwaka 1566 kauli mbiu yake ni Cum cruce et gradio wakiwa na maana ya "kwa upanga na msalaba", kazi yake ni kukusanya na kuchambua taarifa mbalimbali zihusuzo waumini,imani,siasa,teknolojia,karibia kila nyanja wapo. wanakila taarifa ya muumini wao kupitia usajili unaofanya wakati unabatizwa lakini pia kazi yao ya kukusanya taarifa inafanywa kwa weredi na urahisi zaidi maana wanakusanya taarifa kupitia jumuia ndogondogo za kikristo.

ikumbukwe Ignatus luyola hadi anakufa hakuwahi kua padri ila ni mapenzi yake juu ya imani ya kikaktoliki ndio ilifanya akafanya haya, alitamani kuona imani ya kikristo inakua na kua imara zaidi duniani mpaka ukamilifu wa dahari. pongezi za dhati zimwendee kwa kujitoa kwake....Pia bado mada kuu inamuhusu ThomasAquina japo sijamwelezea kwa undani natumani wadau mtaongezea mliyowahi kujifunza kuhusu mtu huyu. kwangu atabaki kua moja kati ya binaadamu wenye akili nyingi waliowahi kuishi duniani. katika orodha ya wanafalsafa kumi yeye anashika nafasi ya sita huku role model wake Aristotle akishika nafasi ya kwanza.
1604961535227.png

-Vinchii
 
'kayafa'.

Hivi hilo neno maana yake ni nini mkuu?Nimeliona linatumika sana sehemu fulani huko mitandaoni.
 
Thomas Aquinas Was Extremely INTELLIGENT....

I commend Muslims to study him....The same task was done by an intelligent and prominent Ulemaa AShaykh ul Kiraam of Zaytuna College, Berkeley CA,shaykh Hamza Yusuf!!

Follow the mentioned Shaykh to understand who was Thomas Aquinas!!!
 
S
Muislim intellectuals wanamsoma sana tu kakini pia hata Thomas moja kati ya watu aliokua anawakubali ni Avecinna huyu jamaa alikua muislim. Aalikua ana maakili balaa nae ni moja kati ya philosopher bora kuwahi kutokea
Sure...The Philosopher Was Charismatic....

Gifted by Almight God!!
 
Muislim intellectuals wanamsoma sana tu kakini pia hata Thomas moja kati ya watu aliokua anawakubali ni Avecinna huyu jamaa alikua muislim. Aalikua ana maakili balaa nae ni moja kati ya philosopher bora kuwahi kutokea
Avicenna kwa Kiarabu ni Ibn Sina hakuwa Muislamu.
 
Nanukuu :

Hii kwa wote wasio mjua Ibn Sina. Yeye ni Aboo ‘Alee Al-Husayn ibn ‘Abdillaah ibn al-Hasan ibn ‘Alee ibn Sina.

Ibn Qayyim al-Jowziyyah, said:

He (Ibn Sina) was from the Qaraamitah Baatiniyyah [Sect], those who do not believe in a beginning (of the creation) nor an end, nor do they believe in a Lord of the creation, nor any prophet sent from Allaah, the Most High.
Such deviant hypocrites (zanaadiqah) pretend to be Raafidhah, whilst they conceal pure, absolute disbelief inwardly, claiming to be descendants of the family of the Messenger (may Allaah raise his rank and grant him and his family peace). He and his family are all free of them in terms of both lineage and religion… [4]
 
Thomas Aquinas Was Extremely INTELLIGENT....

I commend Muslims to study him....The same task was done by an intelligent and prominent Ulemaa AShaykh ul Kiraam of Zaytuna College, Berkeley CA,shaykh Hamza Yusuf!!

Follow the mentioned Shaykh to understand who was Thomas Aquinas!!!
Hawa Wasomi wako huwa vituko sana. Hamza Yusuf naye ni Ulamaa ?

Hivi huwa mnatumia vigezo gani kumjua fulani ni Ulamaa na fulani siyo ?
 
Hawa Wasomi wako huwa vituko sana. Hamza Yusuf naye ni Ulamaa ?

Hivi huwa mnatumia vigezo gani kumjua fulani ni Ulamaa na fulani siyo ?
Jurjani Asalaam aleikum!

Hamza Yusuf Ni Shaykh Ambaye Wewe Binafsi Una mtazamo naye tofauti...kwani angekuwa ni miongoni mwa wale uwapendao kutoka SAUDI ARABIA...wale WAHHABI wala usingempinga.....

Hapa mjadala ni MWANAFALSAFA MTUNDUIZI wa dunia,Hayati Thomas Aquinas....
 
Jurjani Asalaam aleikum!

Hamza Yusuf Ni Shaykh Ambaye Wewe Binafsi Una mtazamo naye tofauti...kwani angekuwa ni miongoni mwa wale uwapendao kutoka SAUDI ARABIA...wale WAHHABI wala usingempinga.....

Hapa mjadala ni MWANAFALSAFA MTUNDUIZI wa dunia,Hayati Thomas Aquinas....
Unajua kuna muda kuacha upotevu unaenezwa ni tatizo kubwa sana. Kuna swali nimekuuliza umelikimbia. Hamza Yusuf ni Sufi na anawaita watu katika Usufi, yaani ni mzushi.

Uliza wanafunzi wakiingia katika madarsa katika chuo cha Zaytun wanafanya matendo gani ?

Yeye anasemaje kuhusu kuwafundisha watu somo la Itikadi ? Sasa sisi tunamkataa kwa upotofu wake na si dhati yake. Yaani anapingana na mafundisho sahihi ya Uislamu.

Tukirudi kwa Thomas,kwangu mimi huyu si mtu mwenye akili, sababu alikosa ala za kuujua ukweli kama walivyo kosa kina Aristoto, Plato na Wanafalsafa wengine.
 
Back
Top Bottom