CV ya John Mnyika

Duh hiyo imetulia sana kwa mbunge wangu wa ubungo, kifupi ukitaka kujua mtu wenye akili we angalie matokeo yake ya form four tu.

Ukikutana na mtu ana PHD then matokeo ya form four ana FOUR ya nguvu basi utajua tu MAGUMASHI.


Una uhakika na hapo ulikazia??..usichukulie watu wawili watatu ukaconclude...
 
Form Four (1998) Maua Seminary div 1 point 7, A (tisa)9, out of 10 subjects!



Maua Seminary ni sawa ila Tambaza na UD umechakachua, Tambaza alipata Div 2 weak na UD alifanya LLB
Sijui nimuamini yupi hapa, labda huyu mwenye sura nzuri NOT ENOUGH, ndio maana huwa napenda kuwepo mwenyewe kwenye matukio.
 
Najua alisoma udsm,ila cjui course gani,kama ni BBA hyo kwa ud ilikuwa ni everning prgram,hasa kwa mature entry,sasa mwenye data za uhakika atupe,ila jamaa ni mzuri.
 
Sasa hapo udsm alisoma LLB or BBA which is which?
 
Jamani mbona sielewi hii cv yake?!mara amepata division 1 ya pts 3 mara amepata division 3 ya mwanzo mara division 2 alipomaliza form six..twambieni ukweli basi acheni kusifia sifia na kupaka mafuta kwenye chupa.nachokumbuka ni kwamba nilikuwa na mnyika udsm 2004 wakati wa mgomo wa kumuondoa kayombo kwenye urais lakini sikumbuki alikuwa anasoma kozi gani, pia wakati huo BBA ilikuwa haijaanza!!
 
Jamaa ni fuvu la ukweli,akiendelea hivi atafika mbali sana.Muhimu ajazie kashule kidogo kidogo maana umri naona unamruhusu sana.
 
TAMBAZA ALIPATA Div 2:10, alikuwa hajatulia na masomo, c mnakumbuka ezi zile za TYVA (Tanzania Youth Vision Association) kipindi kile ziara za nje ya nchi zilizidi. Nakumbuka alikataa kujoin UDSM B.COM FULL TIME APATE MUDA WA KUFANYA MAMBO YAKE ndio akaenda BBA Evening! Kifupi Mnyika yupo safi kichwani!
 

Na pia kwa kuwa Sharp Lady humfahamu vizuri jamaa analipa; jaribu habati yako.......
 
Wanaotaka cv za wenzao waweke zao hapa kwanza tujue. Angalia anafanya vipi kazi CV haikusaidii.
Nawakilisha.
 
Future presidential material ambayo iko silent wala haina papara kama akina Kabwe na Zitto. Nami nampa big up
 
TAMBAZA ALIPATA Div 2:10!


Hivi hawa wanaosomaga seminari kuna siri gani? kutoka div one pwenti seven hadi two , kuna jamaa alikuja shule yetu(
Milambo Wanaume) na pwenti saba zake kutoka maua kichwani alikuwa mupu hadi walimu wakawa wanamtania muuza feki.
 
Mbona kwenye mjengo kule Dodoma huyu Mnyika na wabunge wengi mayanki wamekuwa mabubu na hawashi ule moto kama wa akina Zitto? So far mimi namfagilia Lissu na Zitto
 
Mbona kwenye mjengo kule Dodoma huyu Mnyika na wabunge wengi mayanki wamekuwa mabubu na hawashi ule moto kama wa akina Zitto? So far mimi namfagilia Lissu na Zitto
Mkuu hujaliona bunge jioni ya leo, dogo mkali sana yule. Lisu nae jembe!
 


Hiyo ya form four nakubaliana na wewe kwakuwa Mnyika aliniacha pale Maua seminary lakini Hapo kwenye red umedanganya, alipata div 2 pt 10. Ila ilikuwa justifiable kwakuwa akiwa A level huyu mheshimiwa alikuwa na amjukumu mengi sana mara kadhaa alikuwa hata akisafiri nje ya nje.
 
Hivi hawa wanaosomaga seminari kuna siri gani? kutoka div one pwenti seven hadi two , kuna jamaa alikuja shule yetu(
Milambo Wanaume) na pwenti saba zake kutoka maua kichwani alikuwa mupu hadi walimu wakawa wanamtania muuza feki.


Tatizo ni mfumo wa elimu wa kupewa kila kitu tofauti na shule za serikali, mie nimesoma seminary (maua) o level....A level shule ya serikali, chuo kikuu UDSM na Masters nje ya nchi kwa scholarship (based on merits)....huko kote matokeo yangu ni consistent, nimetandika "As" mwanzo mwisho. Kama unatoka seminary unapaswa ukienda serikali uji-adjust na mazingira la sivyo lazima uumbuke. Mie miaka yote minne niliyokaa maua mwl. wa chemistry alikosa kipindi mara moja tu tena alifiwa, nimeenda serikalini, mwalimu wa GS kaingia darasani mara moja tu miaka yote miwili, sasa hapo ndio uone kivumbi chake, na masomo mengine ni hivyohivyo.
 
Hivi mnafahamu cv za Bill Gates? mkizifahamu hamtapoteza muda wenu wa kujadili makaratasi badala ya upstairs. kama shida yenu ni makaratasi Augustino Mrema nae ni PHD HOLDER. mpo hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…