CV ya Mwinyi Zahera

CV ya Mwinyi Zahera

Kalolelo

Senior Member
Joined
Oct 17, 2018
Posts
164
Reaction score
244
Zahera anakuja Yanga akitokea timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako alikuwa Msaidizi wa Florent Ibenge tangu Sep 30, mwaka jana.

Lakini Zahera pia amezifundisha DC Motema Pembe ya kwao, DRC tangu Machi 1, mwaka 2015 hadi Machi 10, 2016, akitoka kuwa kaimu kocha wa AFC Tubize ya Ubelgiji kati ya Oktoba 7 na Oktoba 23, mwaka 2014 ambayo alijiunga nayo akitoka kuwa Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya DRC kati ya Agosti 14 na 28, mwaka 2017 chini ya Ibenge.

Alikuwa anafundisha AFC Tubize kwa mara ya pili, baada ya awali kuifundisha kama Kocha Mkuu kuanzia Julai 1 hadi Oktoba 20, mwaka 2010.

Zahera Mwinyi alizaliwa Oktoba 19, mwaka 1962 kabla ya kuanza soka mwaka 1975 akiichezea klabu ya Bankin ya Goma, Kaskazini mwa jimbo la Kivu, DRC hadi mwaka 1980.

Baadaye akaenda Kinshasa kucheza soka na kujiendeleza kielimu, akijiunga na Chuo cha Teknolojia (ISTA) huku akichezea klabu ya Sozacom hadi alipokutana na wakala wa wachezaji, Mbelgiji Karl Broken aliyemchukua na kumpeleka Ulaya kucheza soka ya kulipwa.

Mwinyi Zahera alicheza kwa misimu miwili Antwerp FC ya Ubelgiji kabla ya kumaliza mkataba wake na kwenda Ufaransa alikochezea timu za Daraja la Pili, Amiens, Beauvais na Abbeville hadi akastaafu soka.

Baada ya hapo akaanza kupata mafunzo ya ukocha, Zahera Mwinyi ambako alitunukiwa Diploma na leseni A ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kabla ya kuifundisha klabu ya SC Feignies ya Ufaransa kuanzia mwaka mwaka 2000 hadi 2010 kwa mafanikio makubwa kabla ya kwenda Ubelgiji kuifundisha Tubize na baadaye jkutrejea nyumbani.
 
Ukweli Zahera anaweza fundisha, kumotivate na kudiscipline timu. Akipata timu iliyo stable financially na kutimiziwa mahitaji yake, wallah Yanga anacheza soka la ushindani
 
Zahera anakuja Yanga akitokea timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako alikuwa Msaidizi wa Florent Ibenge tangu Sep 30, mwaka jana.

Lakini Zahera pia amezifundisha DC Motema Pembe ya kwao, DRC tangu Machi 1, mwaka 2015 hadi Machi 10, 2016, akitoka kuwa kaimu kocha wa AFC Tubize ya Ubelgiji kati ya Oktoba 7 na Oktoba 23, mwaka 2014 ambayo alijiunga nayo akitoka kuwa Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya DRC kati ya Agosti 14 na 28, mwaka 2017 chini ya Ibenge.

Alikuwa anafundisha AFC Tubize kwa mara ya pili, baada ya awali kuifundisha kama Kocha Mkuu kuanzia Julai 1 hadi Oktoba 20, mwaka 2010.

Zahera Mwinyi alizaliwa Oktoba 19, mwaka 1962 kabla ya kuanza soka mwaka 1975 akiichezea klabu ya Bankin ya Goma, Kaskazini mwa jimbo la Kivu, DRC hadi mwaka 1980.

Baadaye akaenda Kinshasa kucheza soka na kujiendeleza kielimu, akijiunga na Chuo cha Teknolojia (ISTA) huku akichezea klabu ya Sozacom hadi alipokutana na wakala wa wachezaji, Mbelgiji Karl Broken aliyemchukua na kumpeleka Ulaya kucheza soka ya kulipwa.

Mwinyi Zahera alicheza kwa misimu miwili Antwerp FC ya Ubelgiji kabla ya kumaliza mkataba wake na kwenda Ufaransa alikochezea timu za Daraja la Pili, Amiens, Beauvais na Abbeville hadi akastaafu soka.

Baada ya hapo akaanza kupata mafunzo ya ukocha, Zahera Mwinyi ambako alitunukiwa Diploma na leseni A ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kabla ya kuifundisha klabu ya SC Feignies ya Ufaransa kuanzia mwaka mwaka 2000 hadi 2010 kwa mafanikio makubwa kabla ya kwenda Ubelgiji kuifundisha Tubize na baadaye jkutrejea nyumbani.
Anaweledi sana Mwinyi Zahera, angetufaa sana hata national team
 
Mafanikio yepi aliyonayo hata unathubutu kusema national team Ndumbula amewahi kuchukua kikombe gani zahela timu ngapi amezifikisha finali . Kocha huyu si lolote si chochota
Anaweledi sana Mwinyi Zahera, angetufaa sana hata national team
 
Tareeq kwa yote aliyofanya Yanga ktk hali ngumu huyaoni??
Anafundisha, anamotivate, analea kama baba na anadispline.
Huyu cocha anatisha!!
 
sasa huyu si alisema amecheza mpira miaka 20 ulaya kumbe alikuwa mfua jezi
 
Zahera akiacha tabia yake ya kuongea hovyo na vyombo vya habari ni bonge la kocha. Shida yake mdomo huwa unamuwasha sana akiona mic. Mapungufu yake makubwa ni kushindwa kutofautisha anahojiwa na nani Azam TV au Makondeko TV. Sasa hivi kuna magazeti na TV uchwara kibao ambazo hazina waandishi wenye weledi katika tasnia nzima ya vyombo vya habari.

Ni wakati sasa kwa Dr. Msola na Mwakalebela wamjulishe Mwinyi Zahera kuwa yeye ni kocha wa timu kubwa sana Tanzania aachane na hizi TV na magazeti uchwara pia ajielekeze zaidi kuzungumzia timu kiufundi yanayobaki amwachie mtu mwenye kazi yake ya mambo ya habari Dismas Ten. Viongozi waliopita walikuwa wanaogopa kumueleza mipaka yake kama kocha anapozungumza na vyombo vyza habari kiasi akija mgeni leo hawezi kujua Zahera ni kiongozi, msemaji wa timu, mfadhili au msemaji wa timu.
 
Eti akiona maiki mdomo unamuwasha, umenichekesha mkuu. Kweli hilo nalo tatizo
 
Back
Top Bottom