CV ya Profesa Jay (Joseph Haule)

CV ya Profesa Jay (Joseph Haule)

The Shumpeter

New Member
Joined
May 21, 2013
Posts
2
Reaction score
5
Joseph Haule a.k.a Professor Jay (amezaliwa tar. 29 Desemba 1975) ni msanii wa muziki wa hip hop laini kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Professor Jay. Katika Tanzania, Prof. Jay anatazamika kama msanii aliyeweza kuwateka wazee waweze kusikiliza muziki wa Bongo Flava. Hasa kwa kibao alichofanya wakati yupo na kundi la Hard Blasters Crew – Chemsha Bongo.

Professor Jay anatokea kundi la Hard Blasters Crew. Kundi hili ni moja ya makundi yaliyofanya muziki huu ambao hujulikana kama ‘muziki wa kizazi kipya' kukubaliwa na sehemu kubwa ya wa Tanzania.

Maisha ya muziki
Professor Jay alianza shughuli za muziki mnamo miaka ya 90 hivi na alijiunga na kundi la ‘Hard Blasters Crew'(HBC) mnamo mwaka 1994. Mwaka 1995 Jay na HBC walishinda kuwa kundi bora la Hip Hop nchini Tanzania.

Jay na HBC walitoa albamu ya kwanza iitwayo ‘Funaga Kazi' mwaka 2000 Albamu hiyo inaaminika kwamba ilileta mapinduzi makubwa sana ya muziki wa Hip Hop nchini Tanzania.

Albamu hii yenye ujumbe mzito ina nyimbo kama ‘Chemsha Bongo' na ‘Mamsapu' ambazo zilichangia kufanya muziki wa ‘Bongo Flava' kuwa wa kila rika na kupewa heshima. Kabla ya hapo muziki huu ulionekana kuwa ni muziki wa wahuni.


Msanii Binafsi
Professor Jay aliamua kuwa msanii binafsi mnamo 2001 na muda mfupi baada ya hapo akatoa albamu yake ya kwanza iitwayo "Machozi Jasho na Damu". Albamu hii ilivuma haraka sana na kumfanya Prof. Jay kupata tuzo ya kuwa mtunzi bora wa Hip Hop nchini Tanzania kwa nyimbo yake ya ‘Ndio Mzee' kutoka kwenye albamu hiyo. na ikifuatiwa na Nyimbo ya "Piga Makofi na Bongo Dar es Salaam"

Mwaka 2003 Alitoa albamu ya pili iitwayo "Mapinduzi Halisi" ambayo nayo ilishinda tuzo ya Kili Music Awards kuwa albamu bora ya Muziki wa Hip Hop nchini Tanzania kwa mwaka 2003. Albamu hii imebebanNyimbo kama "Zali la Mentali", "Msinitenge," na "Promota Anabeep"
Mwaka 2006 Januari alitoa albamu ya tatu iliyoitwa "J.O.S.EP.P.H". Jina la albamu hii lilitokana na nyimbo iliyotoka Mwanzo kabla ya Albamu kutoka. Nyimbo hii ilichaguliwa kuwa nyimbo bora ya Bongo Flava kwenye BBC na Radio One Awards.

Mpya imewahi kuteuliwa kuwa ni albamu bora ya Hip Hop , Mtunzi bora wa nyimbo za Hip Hop, na Nyimbo bora ya Hip Hop ya mwaka kwenye Kili Music Awards. 2006. "Nikusaidieje". na Baadae Kisima Music Awards ya Kenya ilikuwa Nyimbo bora ya Hip Hop na Video bora ya Hip Hop kutoka nchini Tanzania.

Tuzo Alizopata

  • 1 Kili Music Awards (2003)
  • 2 BBC, Radio One Awards (2006)
  • 3 Kili Music Awards (2006)

Muhtasari wa Albamu

  • 1 Aluta Continua ( 2007 ) Ipo Njiani Kutolewa
  • 2 J.O.S.E.P.H. ( 2006 )
  • 3 Mapinduzi Halisi ( 2003 )
  • 4 Machozi Jasho na Damu ( 2001 )

Education
Standard IV

My take:
CHADEMA mmekula garasha. Sijui kama Prof Jay anajua hata kuandika au kutumia computer.
 
mtaongea mengi sana tu ila 2015 lazma muitwe wakimbizi wa kisiasa nchi za n,gambo huko manake mkikaa bongo lazma tuwanyonge %!£¿&*?@#!!
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kwakweli hata jina la profesa halimfai tena Kumbe ameishia darasa la nne khaaaaaaA
 
P jay bora aendelee kuimba lakini siasa hawezi sababu elimu yake ni sawa na darasa la saba kwa maisha ya siku hizi.Asifikiri kupata ubunge ni kazi ndogo,mwenzake MR SUGU kichwa kile.Asijidanganye sababu SUGU kapata ubunge basi na yeye atapata hizo ni day dreaming.Kaona muziki umemkataa anataka kukimbilia kwenye siasa aandike ameumia
 
Wewe ambae sio garasha umekisaidia nini chama chako?acha kuwa na mawazo mgando wewe, unataka kutuaminisha kuwa,magamba wote ni educated? Au kujiunga na chama lazima uwe na elimu?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
kwani wananchi wanahitaji wataalamu wa computer.?

usiwe mjinga wananchi tunahitaji mwakilishi, mtetezi wetu

matatizo yetu hayapo Kwenye computer.

huduma za afya,barabara,maji haziitaji computer kuzijua.!!
 
Huyu jamaa mamake alifanyaga tukio moja ambalo si la ubinadamu na jamaa alikuwepo lakini alikaa kimya,ni mwaka juzi kwenye ile milipuko ya mabomu 'goms'nyumba yao Ipo kota ukonga ilibomolewa kigae kimoja kwenye kona ya nyumba ambayo hakua na aja ya kugombea mahema ya msaada hi hali kuna wananchi ambao hawakua na ata pakuweka ubavu!!!!!
 
shumpeter umeongea kama gamba kweli, elimu maana yake nini?kwa prof jay anataka kuomba kazi bot? Elimu maana yake ni(tafsiri yangu) maarifa ayapataye mwanadamu kupambana na mazingira yanayo mzunguka. Tuambie shumpeter, je prof. Jay anayo hayo maarifa?
 
Last edited by a moderator:
MOSI-nenda darasani ''MMEKURA''ulimaanisha nini?

PILI-huu ujasiri wa kutathimini ubora wa mtu kwa kigezo cha elimu umeupata wapi.

TATU-Aliyekuambia chadema inabagua wenye elimu na wasiyo na elimu ni nani?

NNE-Habari ya mjini ni kuwa prof J,amejiungana CHADEMA leo 21/5/2013 ,kama hujui habari ndo hiyo.

TANO-Rudi kundini,huko ulipo hutafikia malengo uliyo nayo hata ukiyafikia hayatadumu.acha kupoteza muda ''think big''
 
Kwani stive ngo ngedere ana elimu kiasi gani? Na bado ni m,bunge wa chota chote mamsapu sembuse Haule mwanachama tu wa cdm! We bui bui vp umevurugwa??
 
Acha kujifanya kichaaa wakati una akili timamu na MAJI MALEFU KAFIKA LEVEL GANI YA ELIMU?
 
Tunataka watu wa kukomboa nchi, suala la elimu lipo ccm ndio maana elimu yao ni kuiba na kuuza wanyamapori na kutoa watu kucha na kuuwana kama walivyomfanyia RPC mwanza
 
Back
Top Bottom