CV ya straika mpya matata sana wa Yanga SC

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Hebu tupate kumfahamu Saidi Ntibazonkiza kwa ufupi, jamaa amezaliwa 1 May 1987 kwa majirani zetu hapo Bujumbura Burundi kwa hiyo kwa sasa ana miaka 33.

Kuhusu umri tuache hivyo hivyo tu maana inasemekana Kagame Cup ya 1997 alicheza. Ukipiga hesabu hapo alicheza akiwa na miaka 10.
Mwamba alianza kucheza soka katika klabu ya Vital’O ya Burundi kuanzia mwaka 2003 hadi 2005. Baadaye alihamia Uholanzi na klabu ya NEC ndio ilikuwa ya eneo la jirani na makazi yake kwa hiyo alianza kufanya mazoezi na timu ya vijana.

Baadaye akasajiliwa kwa mkataba wa kudumu na NEC, mwanzoni mwa msimu wa 2006-07 alianza kwa kucheza timu ya vijana lakini baada ya muda mfupi alipandishwa kwenyebtimu ya wakubwa na mnamo November 18, 2006 alicheza mechi yake ya kwanza kwenye Ligi ya Uholanzi dhidi ya Sparta Rotterdam.

Alidumu NEC kwa miaka minne (2006-2010) akiwa amecheza mechi 70 na kufunga mabao nane

Mwaka 2010 aliondoka NEC na kujiunga na KC Cracovia ya Poland ambapo alidumu kwa miaka minne pia kuanzia 2010 hadi 2014 huku akicheza mechi 85 na kufunga magoli 17.

Baada ya hapo akatimkia zake Uturuki na kujiunga na Akhisar Belediyespor ambapo alidumu kwa mwaka mmoja tu (2014-2015), huku akicheza mechi 13 na kufunga goli moja pekee!

Safari haikuishia hapo, mwaka 2015 akajiunga na Caen ya Ufaransa. Alianzia Caen B ambapo alicheza mechi nne na alifunga goli moja. Baadaye akapelekwa Caen ya wakubwa ambapo alicheza mechi 14 na kufunga goli moja kwa mwaka mmoja ambao alicheza hapo.

Baada ya kuondoka Ufaransa, mwaka 2017 akaenda zake Kazakhstan na kujiunga na FC Kaysar Kyzylorda ambayo aliichezea mechi 10 na kufunga mabao mawili.

Baada ya miaka 12 ya kuzunguka Ulaya, akarudi zake nyumbani Burundi kwenye klabu yake aliyoanzia maisha ya soka Vital’O.

Jana ametia dole gumba kuitumikia timu ya WANANCHI Yanga SC.
 
...Baadaye akajiunga na Yanga, na kucheza mechi 10 na kufunga goli moja katika mashindano ya Ndondo Cup (goli lilikataliwa na refa)
Sasa hivi kahamia Tandale kwa tumbo na kufanya ndio makazi yake,

Endelea na wewe....
 
Mbona lete source ya andiko lako
 
Yanga kama kokoro wanajizolea tu
 
Kagame Cup ya Mwaka 1997 ndio kombe gani hilo, unajua Kagame mwaka huo alikuwa wapi?
 
Naona Yanga wameamua kulamba matapishi yao kwa kusajili kikongwe kuliko wote VPL miaka 34!
 

Kagame cup ya mwaka 1997 alicheza akiwa na timu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…