CV za kibongo zinataka nibandike picha, niweke kabila, umri, nina wake wangapi...

CV za kibongo zinataka nibandike picha, niweke kabila, umri, nina wake wangapi...

Buyaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
1,705
Reaction score
1,953
Nchi hii ina sheria against employment discrimination, sasa kwa nini tunafumbia macho hili tatizo la waajiri kutaka kujua personal information za job applicant ambazo zinaweza kusababisha discrimination?

Nitume picha, najijua nina sura mbaya, kwa hiyo sijaomba kazi ya u-model, picha yangu ya nini? Na hii habari ya kutaka niweke umri na mahala nilikozaliwa ya nini, ujue kabila langu ili iweje?

Nchi za wenzetu zimeshaachana na mpango wa kuandika personal biography kwenye resume (CV).

worst-things-to-put-on-resume-fins: Personal Finance News from Yahoo! Finance
 
Kwa kwe;i hata mimi sikubaliani na kitendo hicho. Huo ni ubaguzi kwa 100%
 
dude.. u want a job just do it... usiwabishie
 
siamini kama kuna kitu kama hicho ila yatakuwa hayo ma Nothing GOING On (aka NGOs) yenu tu
 
siamini kama kuna kitu kama hicho ila yatakuwa hayo ma Nothing GOING On (aka NGOs) yenu tu

I think kama sio Tanzania Railways ni Tanzania Airports, mwezi wa pili walitangaz nafasi na wakataka picha!
But I think kabla hujahukkumu, labda tuulize sababu za wao kutaka picha!
 
siamini kama kuna kitu kama hicho ila yatakuwa hayo ma Nothing GOING On (aka NGOs) yenu tu
MSD,NHIF,PSPF,GPSA,SUMATRA,NECTA,THE INSTITUTE OF JUDICIAL ADMIN-LUSHOTO na NIDA-Ni NGO hizo?????
 
dude.. u want a job just do it... usiwabishie
Hapana nawabishia, na nakupinga kwa kila chembe ya uhai wangu, sivumilii discrimination.

Siku nilipohitimu shule aliyetoa commencement speech alituambia "Never accept the status quo." Usikubalikubali mambo kama yalivyolivyo kwa sababu tu yako hivyo na umeyakuta hivyo ndivyo yalivyo.

Nimekutana na watu wengi wanalalamika employment discrimination, mfano mmoja, kuna widely held perception, whether true or not, kwamba NSSF inaajiri dini moja tu. Anaelalamika anaitwa Matiku Lyamungu. Namuuliza, human resources wa NSSF anajuaje wewe dini gani akunyime kazi? Jibu lake, CV za kibongo zina hizi biographicals zinazoweza kutumika ku discriminate job seekers.

Kuombwa picha, kutangaziana kijijini kwetu wapi, na dini yangu, taarifa za kuoa na kuolewa, hayahusiana na kazi yangu, waajiri wa Tanzania wamepitwa na wakati. Usiniambie nataka kazi basi nisiwabishie, nataka kuchangia kubadilisha jamii yangu, sio kazi.
 
Back
Top Bottom