MjumbeOGG
New Member
- May 23, 2022
- 3
- 3
WALIMU TUMEWAKOSEA NINI?
Salam Kwanu
1.Mhe.Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan.
2.Mhe.Waziri Wa Utumishi na Utawapa bora..Jenista Mhagama
3.Mhe.Waziri Wa TAMISEMI...Innocent Bashungwa.
Kwa miaka Zaidi ya Ishirini Walim wa nchi hii wamekuwa wakiwakilishwa na Chama kimoja cha Wafanyakazi kiitwacho Chama Cha Walim Tanzania (CWT).
Mwalim alipoajiriwa tu aliingizwa moja kwa moja katika kuchangia CWT kwani ni Takwa La Kisheria, maana hakukuwa na chama mbadala. Mbaya zaidi sheria inamtaka mwalim ajaze fomu ya kujiunga lakin wengi wameingizwa kwenye makato bila kujaza fomu.(Ushahidi Upo)
Walim Wamekuwa wakipata matatizo/changamoto nyingi sana pasipo kupatiwa majawabu toka kwa CWT kama watetezi wao. Wameshindwa Kuelewa iwapo CWT inafanya Biashara kupitia Michango ya kila mwezi toka kwa walim au wanatetea walim.
Cha kusikitisha zaidi ni kuona baadhi ya Vitu ambavyo Vinasemekana ni mali ya CWT havimnufaishi mwalim.Mfano;
Pamoja na hali yote hiyo Walim wamekuwa wakishiriki ili kusaidia CWT iweze kubadili Katiba yake lakini imeshindikana, na walim walishindwa kukiacha CWT kwani sheria ziliwafunga.
Kwani Sheria ilimtaka mtumishi awe na chama cha wafanyakazi kitakachomwakilisha.
Walimu Mbona wanafanyiwa Ubabe katika Maamuzi?
ONA HAYA.
Mwaka 2015 kuna vyama vya wafanyakazi vinavyowatetea walimu vilisajiliwa na kuruhusiwa kuhudumia walimu. LAKINI walimu wamekuwa wakitishiwa na kukwamishwa wasijiunge na vyama mbadala wa CWT. Kwa nini?
Wakati Sheria Inaruhusu mwalimu kutoka chama kimoja na kujiunga na kingine?
Kwa nini Walimu wameamua Kujiongezea Mshahara kwa kujitoa CWT na kujiunga na vyama mbadala wanakwamishwa?
Mfano.
CHAMA CHA KUTETEA NA KULINDA HAKI ZA WALIMU TANZANIA (CHAKUHAWATA) kinakata shilingi elfu 5 (5,000) kwa mwezi kama ada ya uanachama.
Wakati
CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT) kinakata asilimia mbili (2%) ya mshahara kwa mwezi kama ada ya uanachama.
Sasa basi Kama Mwalimu ataamua kutoka CWT na kujiunga na CHAKUHAWATA atajiongezea mshahara wake kama inavyoonekana hapo chini.
Kama CWT watamkata elf20 kwa mwezi basi akijiunga na CHAKUHAWATA atakatwa elf5 hivyo atajiongezea elf15 kwa kila mwezi.Hilo ni ongezeko kubwa sana.
Kwa nini mnasumbua walimu wameamua kujiongezea TAKE HOME YAO.
Walim wameamua Kwenda na Kuielewa Serikali ya JMT katika Awamu Zote.Ndio Maana wanaamini Vyama Vya Wafanyakazi Vipo Kisheria Lakini Mwamuz wa Mwisho ni Serikali.
Kama Mlikuwa hamjui ni kwamba Hasir za walimu zinatengenezwa na CWT kwa kujimilikisha walim wote wa nchi..Hizo hasira za chuki wanazisambaza,walim wamekuwa wakiwadharau na kuendelea na kazi.
MOJA KATI YA CHUKI NI HII
CWT Imekuwa ikishirikia na baadhi ya watumishi wa serikali wakiwemo, Maafisa Utumishi (HRO) ngazi ya wilaya ili wawakwamishe walim wasiwez kujitoa CWT.
Makatibu wa CWT wilaya na mikoa wamekuwa wakiwarubuni Maafisa Utumishi ( HRO) wafanye yafuatayo.
Sheria Ifatwe Katika Kujiunga na kijitoa katika vyama vilivyopata usajili.
Mwalim apewe uhuru wa kufanya maamuz yake wakat wote ila tu iwe kwa mujib wa sheria za JMT.
Walim Wasipuuzwe Katika Hili kwani Ni Mbinu ya Kuongeza Kipato Chake.
Nawasalim Kwa Jina La JMT.
KAZI IENDELEE.
MWALIMU OG

- Majengo ya CWT kama Mwalimu House.
- Bank inayoitwa Mwalimu.
- Makato ya 2% toka kwenye mshahara wa kila mwezi.
- Rais wa CWT.
- Katibu Mkuu.
- Makatibu mikoa yote Tanzania zaidi ya 20.
- Makatibu wilaya zote Tz zaidi ya mia moja (100)
- Mwenyeviti wa mikoa na Wilaya zaidi ya 120.
Pamoja na hali yote hiyo Walim wamekuwa wakishiriki ili kusaidia CWT iweze kubadili Katiba yake lakini imeshindikana, na walim walishindwa kukiacha CWT kwani sheria ziliwafunga.
Kwani Sheria ilimtaka mtumishi awe na chama cha wafanyakazi kitakachomwakilisha.
Walimu Mbona wanafanyiwa Ubabe katika Maamuzi?
ONA HAYA.
Mwaka 2015 kuna vyama vya wafanyakazi vinavyowatetea walimu vilisajiliwa na kuruhusiwa kuhudumia walimu. LAKINI walimu wamekuwa wakitishiwa na kukwamishwa wasijiunge na vyama mbadala wa CWT. Kwa nini?
Wakati Sheria Inaruhusu mwalimu kutoka chama kimoja na kujiunga na kingine?
Kwa nini Walimu wameamua Kujiongezea Mshahara kwa kujitoa CWT na kujiunga na vyama mbadala wanakwamishwa?
Mfano.
CHAMA CHA KUTETEA NA KULINDA HAKI ZA WALIMU TANZANIA (CHAKUHAWATA) kinakata shilingi elfu 5 (5,000) kwa mwezi kama ada ya uanachama.
Wakati
CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT) kinakata asilimia mbili (2%) ya mshahara kwa mwezi kama ada ya uanachama.
Sasa basi Kama Mwalimu ataamua kutoka CWT na kujiunga na CHAKUHAWATA atajiongezea mshahara wake kama inavyoonekana hapo chini.
Kama CWT watamkata elf20 kwa mwezi basi akijiunga na CHAKUHAWATA atakatwa elf5 hivyo atajiongezea elf15 kwa kila mwezi.Hilo ni ongezeko kubwa sana.
Kwa nini mnasumbua walimu wameamua kujiongezea TAKE HOME YAO.
Walim wameamua Kwenda na Kuielewa Serikali ya JMT katika Awamu Zote.Ndio Maana wanaamini Vyama Vya Wafanyakazi Vipo Kisheria Lakini Mwamuz wa Mwisho ni Serikali.
Kama Mlikuwa hamjui ni kwamba Hasir za walimu zinatengenezwa na CWT kwa kujimilikisha walim wote wa nchi..Hizo hasira za chuki wanazisambaza,walim wamekuwa wakiwadharau na kuendelea na kazi.
MOJA KATI YA CHUKI NI HII
CWT Imekuwa ikishirikia na baadhi ya watumishi wa serikali wakiwemo, Maafisa Utumishi (HRO) ngazi ya wilaya ili wawakwamishe walim wasiwez kujitoa CWT.
Makatibu wa CWT wilaya na mikoa wamekuwa wakiwarubuni Maafisa Utumishi ( HRO) wafanye yafuatayo.
- Kuwazungusha walim waliopelek fomu za kusitisha makato CWT na kujiunga na CHAKUHAWATA ili wakate tamaa.
- Kuwataka walimu ada ya uanachama toka vyama viwili. ambapo ni kinyume na sheria ya utumishi
- Kuwatishia walimu wanaotaka Kujiondoa CWT. Wakisema wanapambana na serikali.