KERO CWT Ubungo wanatulazimisha walimu kuwa kwenye chama. Tunakatwa mishahara kwa lazima

KERO CWT Ubungo wanatulazimisha walimu kuwa kwenye chama. Tunakatwa mishahara kwa lazima

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na uonevu mkubwa sana wa CWT UBUNGO ikilazimisha kuwakata walimu mishahara kama michango ya chama bila idhini ya wahusika Wala makubaliano.

Na hata wanapoomba kusitishwa Kwa michango hiyo hawasikilizwi au kupewa mlolongo mrefu wa namna ya kujitoa au hutolewa ndani ya muda mfupi Kisha hurudishwa tena kwenye makato bila idhini. K

wamba Wana uwezo wa kucheza na mishahara ya walimu wanavyotaka na hakuna ushirikiano unaotolewa na mwajiri dhidi ya malalamiko hayo. Sheria ya kazi na ajira ya mwaka 2004 inamtaka mtumishi kuwamo kwenye chama cha wafanyakazi alichoridhia na si vinginevyo. Lakini imekuwa kinyume Kwa walimu kwani wamenyimwa uhuru na Haki ya kuchagua kuwa wanapopataka.

Tunaomba mtusaidie kufatilia hili swala maana imekua kero kwa walimu wengi ikiwemo Manispaa ya Ubungo
 
Poleni sana walimu
Yani mwalimu anaonewa na kila mtu katika hii nchi sio mtendaji, mwenyekiti mara diwani sahizi mwalimu nae anamuobea mwalimu mwenzake 😄
 
Back
Top Bottom