Cyber crime KWA KISWAHILI NA KWA UREFU ZAIDI

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Cyber crime
KWA KISWAHILI NA KWA UREFU ZAIDI;



Umoja wa Ulaya Waiasa Tanzania Kuhakikisha Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni ya mwaka 2015 Haikiuki Haki za Raia Wake.

Mabalozi wa Umoja wa Ulaya, Ubelgiji, Denmark, Ufini, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia,

Uholanzi, Hispania, Sweden, Uingereza na Mabalozi wa Canada, Norway, Uswisi na Marekani


wanaikumbusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa ilijizatiti kutumia Sheria

ya Uhalifu wa Kimtandao ya 2015 kwa namna ambayo inaheshimu uhuru wa kimsingi na

kushughulikia uwezekano wa tafsiri hasi ya sheria hiyo. Hata hivyo, kesi za kwanza za

matumizi ya sheria hiyo zimeongeza wasiwasi katika ukiukwaji wa misingi ya uhuru.


Mabalozi wana wasiwasi kuhusu kukamatwa hivi karibuni kwa wafanyakazi wa Kituo cha Sheria

na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre) pamoja na vifaa muhimu vya kiufundi,

Sehemu ya 16 ya Sheria ya Uhalifu wa mitandao ikitumika kama rejea. Matukio hayo yalitokea

wakati shirika hilo lilikuwa likiandaa maoni yaliyotolewa na waangalizi wa uchaguzi nchini

kote, kazi ambayo kituo hicho cha haki za binadamu kilipewa kibali na Tume ya Taifa ya

Uchaguzi. Mabalozi wanafahamu kuwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ni mwanachama

wa Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu.


Kama ilivyoelekezwa katika Mkataba wa Demokrasia wa Afrika, Uchaguzi na Utawala, Mabalozi

wanaamini "kuna haja ya kuimarisha waangalizi wa uchaguzi katika nafasi yao, hasa kwa

kuzingatia umuhimu wao katika kuhakiki utaratibu, uwazi na uaminifu wa chaguzi."


Mabalozi wanaisihi Serikali ya Tanzania kuhakikisha utekelezaji wa Sheria ya Uhalifu wa

Kimtandao haisababishi uvunjifu wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi, hasa uhuru wa

kujieleza na kujumuika na haki ya kushiriki katika chaguzi za uhakika na kwamba inaheshimu

misingi ya utawala bora na jukumu la waangalizi wa uchaguzi na mashirika ya kiraia katika

michakato ya kidemokrasia.
 
Habar, naomba kufahamu kuhusu usambazaji wa video kupitia YouTube channel yangu hasa taarifa au matukio ya kweli yanayotokea maeneo yetu!! Mfano nilibahatika kuingia baraza la halmashauri na kurecord video iliyobebatuhuma za jeshi la polisi kuwaonea raia na mengine mengi, je tukio hilo nikitupia YouTube nitaingia hatiani!!!!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…