Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwanaharakati Cyprian Musiba amedai kuwa kuna watu wasiokuwa na nia njema ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikalini, akiwataja kama "wahuni." Musiba ameongeza kuwa mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amejitokeza kama mkosoaji ndani ya Serikali, akisisitiza kuwa si lazima wakosoaji wote watoke nje ya chama, kama vile CHADEMA, bali CCM wenyewe wanapaswa kukosoana na kurekebishana pale panapohitajika.
Kwa mujibu wa Musiba, Mpina anatekeleza majukumu yake kwa kufuata Ilani ya CCM, ambayo inaelekeza viongozi kuwajibika kwa wananchi na kukosoa pale penye mapungufu. Hii inamaanisha kwamba kukosoa serikali si jambo la vyama vya upinzani pekee, bali hata wanachama wa chama tawala wanayo haki ya kutoa maoni yao na kushauri njia bora zaidi za uendeshaji wa Serikali.
Soma zaidi:
==> Luhaga Mpina kufungua Kesi zote ndani ya masaa 24
==> Mpina: Mzee Kikwete Mwaka 2012 alikataa Mimi kufukuzwa CCM, mimi ni MwanaCCM kwa kuzaliwa siyo kujiandakisha!
==> Dkt Nchimbi: Tofauti ya Mpina na WanaCCM au Wabunge wengine ni tofauti ipo kwenye Familia yoyote