Pre GE2025 Cyprian Musiba: Wasanii tumieni nguvu kubwa kutangazwa mazuri ya Rais Samia

Pre GE2025 Cyprian Musiba: Wasanii tumieni nguvu kubwa kutangazwa mazuri ya Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

McLaren

Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
53
Reaction score
78
Mwanaharakati huru, Cyprian Musiba, amewataka wasanii wa Tanzania kutumia ushawishi wao kutangaza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na Jambo TV jijini Dodoma tarehe 3 Machi 2025, Musiba amesema kuwa kuelekea Uchaguzi Mkuu, ni muhimu kuweka nguvu kubwa katika kusambaza taarifa kuhusu mafanikio ya Rais Dkt. Samia, huku akibainisha kuwa wasanii ni miongoni mwa watu wanaopaswa kushiriki kikamilifu katika jukumu hilo.

Hata hivyo, kauli yake imekuja miezi michache tu baada ya yeye mwenyewe kueleza kuwa haoni umuhimu wa wasanii kushiriki katika matukio ya kiserikali, na kuwashauri Watanzania kuwapuuza.

 
Back
Top Bottom