D.B. Cooper: Tukio halisi la kusisimua lililogeuka hadithi ya 'Alfu lela ulela'

Aisee umemjibu kwa busara sana
Ila watu kama Hawa wapo Kila kitu wanaponda mwache Na yy akaandike tukasome kwake yaani binadamu sijui tukoje!!!!!
 
Aisee umemjibu kwa busara sana
Ila watu kama Hawa wapo Kila kitu wanaponda mwache Na yy akaandike tukasome kwake yaani binadamu sijui tukoje!!!!!
Kuna binadamu waki tu hvo siku zote. Kazi yao kubisha bila hata fact zozote.
 
weka historia yake wengine hatuijui mkuu
babu mapunda John Dillinger alikuwa mwizi wa mabenk na kutoroka Jela za USA Lakini hatimaye aliuawa, tofauti na DB Cooper ambaye hakukamatwa wala haijulikani pesa ipo wapi au hata yeye.
sema page hii ni ya The Bold na story yake akitokea mwenye kujua tafsiri sahihi ya true picture hiyo atatuwekea lkn link ni hii
https://www.fbi.gov/history/famous-cases/john-dillinger
 
Kitu cha muhimu katika hili ni kjifunza ,wenzetu walijifunza katika tukio hili na kuweka mikakati mipya katika usafiri wa anga ,ni bahati mbaya sana /ujinga kwetu huwa hatutumii matukio kama haya kujifunza hebu fikiri kuna tofauti kati ya ajali ya Mv Bukoba na Ajali ya nungwi.............Hatukujifunza nina hakika itatokea tena mbeleni.
 
Anzisha uzi wako basi ili nawew upate wafuasi wako ambao wanaamin uzi huu umekosewa sisi tumeelewa na hatuitaji nyongeza zaidi ya hapa maana hakuna faida tunayopata zaidi ya burudani tu
 
weka historia yake wengine hatuijui mkuu
Me sio mzuri wa kuhadithia kama mkuu wa huu uzi ila kwa kifupi ni huyu jamaa John Dilinger alikua anavamia bank katika imiji tofauti tofauti huko marekani katika miaka ya 1920s na alikua kila akikamatwa kuwekwa gerezani anatoka kwa njia tofauti tofauti. Alisumbua police wa states mbali mbali hadi nchi ikaunda kikosi kazi cha kumuwinda kwa muda mrefu sana, inasemekana kikosi hiki ndicho mwanzo wa FBI. Mbinu ziliwaishia lakin walifanikiwa kumuundia mtego wa mwisho kwa kumtumia mwanamke ambaye John alimpenda sana na aliuwawa wakati akitoka kwenye jumba la cinema mwaka 1934.. kwa kifupi ni hivo
 
Mie pia nawaza hivyo ila kizungumkuti ni wapi hizo hela zilitumika??hilo ni swali linalochanganya akili
 
Mkuu nimekuelewa sana... Hii kitu kaingiza uongo wa wazi kabisa na bado kuna watu wanataka ukae kimya!
 
Mkuu nimekuelewa sana... Hii kitu kaingiza uongo wa wazi kabisa na bado kuna watu wanataka ukae kimya!
Well, thank you, lakini tatizo nadhani hakuelewa kilichosemwa kwenye chanzo chake, ambacho ni Wikipedia, by the way.

Ukisoma alichobandika kama uthibitisho wa madai yake utaona ni tafsiri potofu ya alipokitoa. Kwa mujibu wa chanzo chake:

"Cooper knew how to control its air speed and altitude without entering the cockpit..."

Msimulizi wetu katafsiri:

"Pia Boeing 727 ilikuwa na ubunifu mwingine adhimu tofauti na ndege nyingine kwa kuwa ilikuwa unaweza kucontrol speed na mwinuko wa ndege 'manually' hata ukiwa katika sehemu ya kukaa abiria..."

Kitu ambacho si kweli, hakuelewa halafu akataka kukoleza radha. D.B Cooper ali control uendeshaji ndege kwa instructions au masharti ya maneno kwa marubani, mwandishi wetu ameongeza maneno ya ku control ndege "manually..." Cooper haku control ndege manually wala hakuna panaposemwa hivyo kwenye chanzo chake, na wala haingewezekana.

Cooper alikuwa anaijua ndege vizuri kiasi cha kuweza kutoa maelekezo ya nini kifanyike, badala ya yeye mwenyewe kuingia kwenye cockpit ambako angeweza kuzidiwa nguvu, lakini ndege haikuwa na uwezo wa kuendeshwa "manually" kutokea nyuma kwa abiria.

Na pia suala la ndege hii kuchaguliwa kwa sababu kuruka mwisho ni futi 10,000 hilo nalo alitafsiri vibaya, japo lilichangiwa pia na nia ya msimulizi, again, kutaka kuongeza mdalasini na tangawizi kwenye mchuzi. Ndege ya Cooper ilikuwa na jet engines tatu, hizi huwa haziko comfortable ku cruise chini ya 30,000ft angani.

Mwisho wa siku lakini natumai msimulizi wetu siku nyingine atakuwa makini akiwa mbele ya hadhara ya dunia nzima.
 

Iam sorry mate. Mimi kama msomaji nikiangalia uandishi wako na yeye. I may say mleta uzi Anna credibility kuliko wewe. In nadra sana kuandika story ndefu na ya kusisimua Kama hii ukose makandokando. In all I agree critics daima tupo na tuna kazi ya kuweka mambo sawa. Ila give credibility where it is due. Usicheze sana na semantics.
 
In nadra sana kuandika story ndefu na ya kusisimua Kama hii ukose makandokando. In all I agree critics daima tupo na tuna kazi ya kuweka mambo sawa. Ila give credibility where it is due. Usicheze sana na semantics.


Kitendo cha wewe kusema "give credibity where it is due..." badala ya "give credit where it is due..." inakuondolea sifa zote za kusimama ku challenge ninachosema, kwa sababu unaonekana hujui unachoandika. Huwezi kumpa mtu credibility, unampa credit. Lakini nitakuvumilia.

Okay, now, kama unakubali kwamba hadithi huwa hazikosi makandokando na "critics daima tupo na tuna kazi ya kuweka mambo sawa..." sasa unachonipinga ni nini? Hueleweki. Nimekosea nini kufanya hicho ambacho unasema huwa kipo daima na kinafanywa na critics?

Kitu kimoja namsifu msimulizi ni kwamba anajua ana deal na hadhara ya aina gani, watu kama wewe, light weights wasiojishughulisha sana na kuchambua mambo.

Lazima uwe na confidence na knowledge ya hadhara yako kuweza kuwadanganya kwamba jet aircraft yenye engine tatu hairuki zaidi ya futi 10,000. Nchi ambayo hatujalelewa katika mambo ya ndege ndege anajua hakuna atakaefuatilia na kujua anapotosha.

Hatuna mambo ya vipimo vipimo kwenye jamii yetu. Maharage sokoni tunapima kwa vibaba, kibaba ambacho hakuna mtu yeyote anaejua volume ya kibaba ni nini. Shule una qualify kuanza kama una mkono mrefu wa kufikia sikio la upande wa pili. Lakini kipimo cha urefu wa mkono relative to half the circumference ya kichwa hakuna mtu duniani anaekijua. Mwalimu hajui, mtoto hajui, mzazi hajui, mwalimu mkuu hajui. Lakini ndio kilikuwa kipimo cha ukomavu wa akili kuanza shule.

Kwenye hadhara kama hiyo ukiongea mambo ya altitudes za ndege kuruka angani unawachanganya tu, you can take the whole society on an air ride, say anything you want.

Ndio maana mkikosolewa mnashtuka, mnaghafirika, mnatukana, mnakimbia. Haya ni mambo ya kisayansi, hayataki hasira.
 
ni simu
ni simulizi iliyojaa utata kama kama bermuda triangle huko nako stori kama hizi mara ndege kupote bado kuna utata uliojaa kusadikika na hakuna anayejua kuwa kinafanykikaje wala kutokeaje du, anyway kwa kuwa ni nadharia huenda hayo mambo aidha CIA au FBI walihusika kwa hiyo mambo mengine yalifanyika baadaye ili kupata fund kwa ajili ya kuendesha mambo yao hilo tukio lilikuwa mtaji kwa FBI na CIA
 
Quite a story. Sikuwahi kuifatilia kabla ya hapa(sijui kwanini), so siufahamu mkasa huu, ila kuna vitu kadhaa vinanifanya nijiulize authenticity ya hii story kutoka kwa msimuliaji. Kwanza, Fernando Sucre hakuwa mexican, bali Puerto Rican. Na umuhimu wa Sucre kwenye escape plans za Michael, ulikuja ni kwa sababu wana-share cell, which mean't for Michael to dig out, his cell-mate had to be involved, period.

Anyway, ngoja nikaichimbe mwenyewe. Thanx tho.
 
HAPA watu wanataka wasikike au waonekane wanajua. hii habari mtu haitaki akae kimya, yametolewa machapisho na vipindi kwenye tv za wenzetu zinazoonyesha vipindi vya ukweli kama 'FBI FILES'. mimi nimefatilia hiki pikindi, walitoa habari hii kama ulivyo andika, kwangu nachukulia kama umetafsiri ili wajue wengi,
ILA NI YA KWELI.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…