D-DAY. Nini kilitokea.........

Evvy jr

Senior Member
Joined
Apr 23, 2017
Posts
148
Reaction score
189
Operesheni Neptune au D-Day kama wengi wanavyoifaham (jina la operesheni ya awamu ya kwanza ktk utekelezaji wa Operesheni Overlord) lilijumuisha Marekani, Uingereza, Canada, Ufaransa na vikosi vingine vilivyompinga Adolf Hitler.

Hatua tano za uvamizi ziligawanyika kati ya majeshi ya Marekani na Uingereza; Beach ya Utah na Omaha zilipangiwa jumla ya askari karibu 73,000 wa Amerika, na kazi yao ilikua kupigana kuelekea kilele cha Pointe du Hoc katikati ya pwani ya Omaha. Fukwe tatu zilizobaki ni Sword, Gold, na Juno zilichukuliwa na kugawanywa kwa wanajeshi wa Uingereza na Canada. Maeneo yote haya yalikua ni sehemu ya Ufaransa ambayo yalikua yameshikwa na askari wa Ujerumani.

Leo tutaangalia kwa makini maeneo haya 5.

GOLD
Kuwasili Gold Beach ilipangwa iwe saa 7:25 asubuiJuni 6, 1944, tofauti ya saa moja baada ya Wamarekani kufika Utah na Omaha. Tofauti ya wakati iliwekwa kutokana na tofauti ya mawimbi ya bahari katika fukwe hizi. Upepo mkali wa bahari pamoja hali mbaya ya hewa kuliifanya operation hii kuwa ngum kuliko ilivodhaniwa. Kwa bahati nzuri, athari nyingi ziliepukika kutokana na usaidizi wa mashambulizi ya ndege za HMS Ajax, na HMS Argonaut, ambazo zilipunguza kasi ya mashambulizi ya wanajeshi wa Hitler kuelekea pwani ya Omaha na Gold.

Wakati huo huo, askari wa miguu walikuwa wamefika tayari na walipigana njia kwa njia pamoja nakukutana na vikwazo vilivyowekwa pwani. Seargent Company ndiye aliongoza vikosi hivyo kwa weredi mkubwa. Wajerumani walishindwa vibaya huko Gold na hawakuwa na jinsi iliwabidi wasalim amri. Takribani askari 350 walipoteza maisha na wengine zaidi ya 1000 walijeruhiwa



JUNO
Kama ilivokua huko Gold beach hali ya hewa katika Pwani ya Juno haikua nzuri, hivyo askari wa miguu walifika kwenye pwani kabla ya vifaru na siraha zingine nzito kufika. Hii ilisababisha wapate upinzani mkali kutoka kwa Wajerumani na wengi walipata majeraha makubwa katika dakika za kwanza za mapambano. Pia, mabomu mengi yalishindwa kulenga shabaha ktk sehemu muhimu hivyo vikosi vya ulinzi vilitumia zaidi uwezo wao wakati wa shambulio hilo.

Kikosi namba 9 cha askari wa miguu wa Canada kilifanya ufanisi mkubwa siku hiyo, kilipigana mpaka kufikia karibu na uwanja wa ndege mdogo katika kijiji cha Capriquet. Majeruhi ya 961 pamoja na maiti za askari 340 zilipatikana katika pigano la siku hiyo



SWORD
Kwa Sword Beach, vifaru 21 kati ya vifaru 25 viliweza kufika pwani, hivyo viliweza kutoa msaada mkubwa wa mashambulizi kwa askari wa miguu na wakaweza kusonga mbele, ingawa kulikua na msaada wa vifaru lkn pwani ilikua na vikwazovingi na vya hatari na kufanya kazi iwe ngumu na hatari kwa kikosi kilichohusika.

Vikosi vya Ufaransa chini ya Kamanda Phillipe Kieffer waliwasili Sword pamoja na vikosi vya Uingereza. Walikuwa na jukumu la kukamata sehem muhimu kabisa ya wajerumani RivaBella katika kijiji cha Ouistreham ambako kulikua na mizinga iliyokua ikitumiwa na Wajerumani. Komando mmoja wa jeshi la Waingereza alifanikiwa kuuteka mnara unaosaidia kutoa ulinzi mahali hapo na kufanya operation kuwa rahisi.
Askari wa Uingereza walizidi kusonga mbele na kuendelea kushikilia maeneo mengine muhimu kuelekea ktk mji wa Caen.


Itaendelea......
 
Naisubiri kwa hamu sana mkuu.Imekaa njema sana
 
Be the second to reply

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
D day landing..... Historia nzuri, amani haiji Ila kwa ncha ya upanga. Hitler alikuwa hatari kwa dunia yetu.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Natamani hii kitu ingekuwa movie.....hizi ndio muvi zangu napendaga...by the way....Pokea LIKE mleta maada
 
"Aaaah kijana umenikumbusha mbali tulipokua tunapambana huko burma" watakuja tu na wa burma hii ndo jf bwanaaa
 
Naona unataka kurithi mikoba ya The Bold...well done mkuu
 
hitler alikua mtata sana yule kiumbe

sent from my iphone 7 nimeinunua SAPNA pale POSTA
 
Cheza game lake liko play store.


Game moja zuri sana,kuanzia graphics,sound na hata ugumu wa mission yenyewe,nashauri pia atafute picha moja ya kivita inaita "Furry"ama furious,zte zimejaribu kuelezea nini kilitokea wakati huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…