BigBro, kwa kiasi kikubwa, Marekani (na pia nchi zingine zilizoendelea) wanachukulia michezo kama njia nyingine kubwa ya ajira na kuendeleza uchumi. Nimekaa Marekani miaka 20 sasa na nimegundua yafuatayo. Kwa mfano, michezo inaendelezwa tokea watoto wako wadogo sana hususani kwenye Basketball, Baseball, American Football, Hockey, Track and Field, Golf, etc). Kwa kiwango kikubwa, shule karibu zote zina viwanja vya hiyo michezo vya viwango vya juu. Halafu wakati Tanzania imesimamisha mashindano ya Umisseta (binafsi nilishiriki mara mbili miaka ya mwanzoni mwa tisini), Marekani kuna mashindano ya mashule kila mwaka ya kutoka kitongoji unachoishi, kwenda kwenye majimbo na kuishia nchi nzima (School District championship, State championship, NCAA, etc). Hii inaimarisha michezo kwa kiwango cha juu sana. Pia shule zinaimarishwa sana na kodi wananchi wanazolipa kwa kujenga viwanja na kununua vifaa vya michezo vya kisasa. Hali kadhalika, mashirika makubwa kama Nike, Under Armour, Coca Cola, Pepsi, etc yanafadhili sana shule pamoja na wanamichezo. Kwa mfano, wanamichezo wa viwango vya juu kama Michael Phelps wanapata udhamini wa makampuni mengi sana. Kwa hio yeye kazi yake ni kujiandaa kwa miaka mine kwa ajili ya Olympics. Haishangazi sana wanapopafanya vizuri na kupata medali nyingi.
Pia nchi hizi wanachukulia michezo kama mfumo mzima wa wananchi wake kupata kazi na kama chanzo cha kupata mapato ya kodi. Kuna mfumo mzima ulianzishwa kutokana na michezo. Kuna wanamichezo, mawakala, wanasheria, madaktari, wawekezaji kwenye michezo, etc wanaoajiriwa kutokana na michezo bila kusahau vitega uchumi vya miundombinu (sports infrastructure). Watu wote hao wanalipa kodi kwahio nchi inafaidika sana na kodi hio. It's a win-win situation for both parties (athletes and the government).
My 2 cents.