Da! Kila Olimpiki Marekani ndo inaongoza kwa Medali

Maandalizi ndugu yangu sasa kuna michezo mingine ndio kwanza tunaiona kumbe kwa wenzetu ina muda mrefu sasa hata ukija hiyo tunayojifanya tunaijua ni ubabaishaji jazz band usanii si usanii magumashi si magumashi hatuna u tayari ni blah blah
 
Màandalizi muhimu na uwekezaji kwenye michezo, tofauti na bongo wizara hata haijui majukumu yake tuna force mpira ambao hautatifikisha popote.
 
BigBro, kwa kiasi kikubwa, Marekani (na pia nchi zingine zilizoendelea) wanachukulia michezo kama njia nyingine kubwa ya ajira na kuendeleza uchumi. Nimekaa Marekani miaka 20 sasa na nimegundua yafuatayo. Kwa mfano, michezo inaendelezwa tokea watoto wako wadogo sana hususani kwenye Basketball, Baseball, American Football, Hockey, Track and Field, Golf, etc. Kwa kiwango kikubwa, shule karibu zote zina viwanja vya hiyo michezo vya viwango vya juu. Halafu wakati Tanzania imesimamisha mashindano ya Umisseta (binafsi nilishiriki mara mbili miaka ya mwanzoni mwa tisini), Marekani kuna mashindano ya mashule kila mwaka ya kutoka kitongoji unachoishi, kwenda kwenye majimbo na kuishia nchi nzima (School District championship, State championship, NCAA, etc). Hii inaimarisha michezo kwa kiwango cha juu sana. Pia shule zinaimarishwa sana na kodi wananchi wanazolipa kwa kujenga viwanja na kununua vifaa vya michezo vya kisasa. Hali kadhalika, mashirika makubwa kama Nike, Under Armour, Coca Cola, Pepsi, etc yanafadhili sana shule pamoja na wanamichezo. Kwa mfano, wanamichezo wa viwango vya juu kama Michael Phelps wanapata udhamini wa makampuni mengi sana. Kwa hio yeye kazi yake ni kujiandaa kwa miaka minne kwa ajili ya Olympics. Haishangazi sana wanapofanya vizuri na kupata medali nyingi.
Pia nchi hizi wanachukulia michezo kama mfumo mzima wa wananchi wake kupata kazi na kama chanzo cha kupata mapato ya kodi. Kuna mfumo mzima ulianzishwa kutokana na michezo. Kuna wanamichezo, mawakala, wanasheria, madaktari, wawekezaji kwenye michezo, etc wanaoajiriwa kutokana na michezo bila kusahau vitega uchumi vya miundombinu (sports infrastructure). Watu wote hao wanalipa kodi kwahio nchi inafaidika sana na kodi hio. It's a win-win situation for both parties (athletes and the government).
My 2 cents.
 
Tanzania ni kinyume chake.

Kaka ...
 
Wenzetu wana maandalizi mazuri na exposure pia kwa wanamichezo wao ila sisi huku ni majungu na kukatishana tamaa tena na serikali yenyewe acha kenya waendelee kutesa kwa Afrika mashariki na bara zima la Afrika mana wamewekeza kwenye riadha na matunda yake wanayaona ila sisi hata mchezo mmoja unaotutoa kimasomaso haupo
 
Kwa wenzetu michezo wanaithamin sana, sababu wanajua kupitia michezo wanatengeneza nafasi nyingi za ajira, pili ni njia nzuri ya kutangaza Nchi, wakati sisi tunasubiri mtu atokee huko aliko ndio tuanze kuhangaika nae, wao wanaanza kuandaa vijana wao kuanzia wakiwa wadogo. Sasa watu wa namna hiyo unaanzia wapi kushindana nao!!
 
Bila mipango na uwekezaji wa maana tutaendelea kuwashangilia wenzetu tu kila siku. Kuna mwanadada nilimwona jana anaiwakilisha Germany, baba Mtz mama Mjeru, ila ameamua kuiwakilisha Ujerumani
 
Sisi tunadeal na ukawa kwanza tukishawadhibit ndo tutaangaliaga mambo mengine hayo
 
Maandalizi ndugu yangu sasa kuna michezo mingine ndio kwanza tunaiona kumbe kwa wenzetu ina muda mrefu sasa hata ukija hiyo tunayojifanya tunaijua ni ubabaishaji jazz band usanii si usanii magumashi si magumashi hatuna u tayari ni blah blah
Kwa kweli hata mie baadhi ya michezo nimeiona juI.........sie bado sana aisee.....na huu mpira wa simba ya yanga bado ni magumashi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…