Daaah! Mke wa mtu noma aisee!

Daaah! Mke wa mtu noma aisee!

Abbasfarudume

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2017
Posts
1,625
Reaction score
1,326
Wakuu habari zenu wote kiumjula, bila ya kupoteza muda. Rejea kichwa cha habari hapo juu kinavyosema, nakumbuka mwaka huu mwezi wa 7, nilienda wilayani liwale mkoa wa lindi. Sasa wakati huo nina kama siku tatu tangu nifike liwale, na safari yangu ilinichukua wiki nzima hapo liwale. Sasa nakumbuka siku hiyo mida ya saa 8 kamili mchana, nimekwenda stand kuu, ya liwale kwenda kupata lunch, mgahawani sasa pale nikakutana na, mwendawazimu wa kiume mkaka wa makamu hivi mwenye umri wa miaka, kama 40 hivi kavaa juu blauzi, mdomoni kapaka rangi ya mdomo "Shedo" kavaa sket, na alikuwa kaweka mtandio begani, nywele zake kasuka mabutu, hadi mwendo wake anatembea kama mwanamke, alafu alikuwa kachafuka kichizi mwilini, Yaani Chizi kwisha kazi. Sasa mie nikawauliza wenyeji wa pale, hili nijue maswahibu gani yaliompata, yule jamaa mpaka akawa hivyo. Wenyeji wakanieleza yule Jamaa alikuwa nzima kabisa, hila alikuwa anatembea na mke wa mtu, mwenyewe mwenye mali, alipomgundua. Akamwambia wacha kutembea na mke wangu, jamaa akamjibu kwa jeuli, dharau, matusi, na kashifa juu. Mwenye mali akasema isiwe tabu, akamwambia Utaona! Basi mwenye mke akaenda kwa Babu wa Loliondo, kumtengeneza jamaa Akapata Uchizi, hadi anaokoteza chakula kwenye mapipa ya takataka pale, stend Liwale anakula>>>>>>>ANGALIZO TUEMUKANE NA WAKE ZA WATU MKE WA MTU NI SUMU, NA WANAWAKE EPUKANENI NA WAUME ZA WATU MTAOKOTA, MAKOPO BARABARANI!
 
Wapendwa muwe na Usiku mwema, na njozi njema mungu akipenda tutaonana tena asubuhi, panapo uzima na majariwa yake mwenyezi mungu, akituamsha salama alamsik.
 
Inasikitisha sana...


Kwa upande mwingine jamaa alitakiwa a-deal na mke wake... Kwa nini akubali kwenda kufanywa na mwanaume mwingine, wakati anajijua ni mke wa mtu...



Cc: mahondaw
Ibilisi shetan, Ukimpa nafasi anakutawala mkuu.
 
Inasikitisha sana...


Kwa upande mwingine jamaa alitakiwa a-deal na mke wake... Kwa nini akubali kwenda kufanywa na mwanaume mwingine, wakati anajijua ni mke wa mtu...



Cc: mahondaw
Sasa ningemtia uchizi mke wangu watoto ningelea na nani?

Bora sasa hivi wajinga wajinga hawamsogelei nishawapa case study ya kuiconsider wakijiona wanamtaka mke wangu.
 
Back
Top Bottom