Dada huyu anaomba Msaada wenu kimawazo .....

FirstLady1

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2009
Posts
16,789
Reaction score
5,401
Wana JF
Huyu ni mama wa 2 kids
Mtoto wa kwanza alimzaa na mwanaume mwingine miaka 6 iliyopita ,yalitokea matatizo hawakuweza kuwa an uhusiano na huyu baba wa mtoto na akawa ameoa,Ila katika kipindi chote hicho Baba wa mtoto hakuwahi kuwasiliana na huyu dada wala kutoa matumizi ya mtoto wala kukumbuka kama aliwahi kuzaa dada alisononeka mpaka akazoea
Mungu si Athuman huyu dada nae akapata mwenza na akafunga ndoa mwaka jana.wanaishi na mmewe kwa amani na upendo na mungu kamjalia mtoto mwingine ana 6 month sasa.
Tatizo limeanza baada ya huyu mzazi mwenzie kufukuzwa kazi ,pia biashara zake zimefirisika sasa hana kitu kabisa amerudi kwa mama mtoto wake huyu na anabembeleza asaidiwe angalau aanze tena maisha na ameanza kumlaumu eti ajaribu kukumbuka fadhira alizomfanyia kipindi walipokuwa B/F na G/F na anaomba asahau tofauti zao
Mbaya zaidi huyu Baba mtoto wake kaanza kupiga simu na kutuma msg za malalamiko mpaka usiku wa Manane
Huyu dada ana hofu kama mmewe akijua kinachoendelea ndoa yake iko matatani ,kamuelewesha huyo baba wa mtoto wake lakini inaelekea haelewi na amekuwa king’anga’nizi
Anajiuliza amwambie mmewe au afanyeje maana jamaa haachi usumbufu
Kila anapojisikia anapiga simu na kutuma msg .

Pls msaada wenu kimawazo kwa dada huyu
 
alimpa namba yake ya simu ya nini naye???...kama alimuacha siku nyingi na hakutaka kujua lolote kuhusu yeye means hakuwa hata na contact naye...au ametafuta mawasiliano kutoka kwa rafiki zake? kama ni hivyo hawakumueleza sasa kama ameolewa?...mnh
 
Hili nalo ni la kuomba msaada? How far can she handle the disturbances?
 
If a crap is crapping.....kindly amshauri aje kumwomba 'mzee' mwenyewe...then amtaarifu 'mzee'!
 

Kwakuwa tayari yupo kwenye ndoa, so mumewe anajua kuwa alizaaa na mtu mwingine. ni suala la kusema kwa mumewe juu ya mawasiliano yaliyopo na huyo Baba wa mtoto. na ikiwezekana awakutanishe ( kwa simu au ana kwa ana), ni jambo la kawaida kama umeamua kufunga ndoa na mtu aliezaa. Hilo litamtia adabu huyo mwanaume, na hapo huyu dada atajua kama shidaza huyo mwanaume zina zinaukweli au la . kwa maoni yangu huyu dada amesha msaidia sana huyo bwana kwa kumlelea mtoto, sasa anaporudi tena kuomba msaada ilihali bado anasaidiwa kulelewa mwanae , ni kukosa shukurani.
 
Amwambie huyo mume wake mapema na asimfiche chochote.
Mambo yakiharibika zaidi patakuwa hapatoshi.
Wanaume wengine bwana...aaaahgggrr.
 
Ni vizuri amuambie mumewe,hivi maana ya mume ni nini kama hamshirikishani magumu kama haya?mumewe aweza kuwa wa msaada sana kwa mkewe kwenye hili.....nafikiri huyu dada awe na boundaries,she is married for God's sake,yanini kuwasiliana na X kiasi cha kujadili hadi fadhila za zamani na kuwa sasa kafilisika anahitaji msaada......kajiachia sana na hili litamgharimu akicheza........

Mumewe atagundua tu siku si nyingi,kwa kuwa huyu dada pia anajua analofanya si sahihi na hilo litajionyesha tu....amshirikishe mumewe na akate mawasiliano na huyo mwanaume wa zamani.....let the past remain the past!!!!
 

Huyo mtoto ni wa baba aliyetosa au wa mama ambaye amemzaa na kumlea mwenyewe?

Duh hiv mtoto ni wa baba au/na mama?
 
Huyu mwanaume nae ana matatizo kama hakumjua dada wa watu katika shida iweje yeye apate shida aanze kutoa lawama ,majitu mengine myuzzzzzzzzzzzzzzz
 
Katika hali ya kibinaadamu, kama unahisi una uwezo wa kumsaidia, wewe msaidie tu bila kujali alikufanyia nini hapo awali. Maisha yanaenda yakibadilika. Kutokana na ugumu wa maisha, kuna uwezekano mkubwa sana huyo bwana akawa amebadilika. Msaidie tu, inawezekana baadaye akaja kutoa contribution kwa mtoto wenu. La msingi ni kwamba, usije ukafanya siri kwa kila hatua ya msaada utakayoichukua. Mweleze mumeo kila kitu!
 
Huyu mwanaume nae ana matatizo kama hakumjua dada wa watu katika shida iweje yeye apate shida aanze kutoa lawama ,majitu mengine myuzzzzzzzzzzzzzzz

umesahau hawa viumbe wanasahau kirahisi sana?sishangai,ila wanakera.......!!!!
 
Hii inaonyesha dhahiri bado unampenda. Km humwitaji badisha namba yako cm kwa kufanya hivyo utainusuru ndoa yako
 
Bold: ndo jibu:coffee:
 
Huyo mwanaume wala asimpe kipaumbele kabisa, nashangaa hata anataka kushauriwa nini, yeye asimpe chance akaharibu ndoa yake sababu alisha amua kuachana nae na kuolewa na mwingine. Unajua wanawake tunajisahau na huruma zetu hizi zitacost maisha yetu, embu fikiria mpaka maisha yamempiga ndio anakukumbuka ina maana yangekuwa safi hata tusingesikia hii story. please dada wala usimpe nafasi huyo mkaka.
 
Huyu mwanaume nae ana matatizo kama hakumjua dada wa watu katika shida iweje yeye apate shida aanze kutoa lawama ,majitu mengine myuzzzzzzzzzzzzzzz

Ndo najiuliza kwa mtaji huu, nikisema siwapendi wanaume wa jinsi hii nitakuwa nimekosea??
Hivi kweli huyu dada anahangaisha kichwa chake na crap kama huyu!!

Mungu amekupa mume, unataka ubomoe ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe?
Dada simama kwa miguu yako kumkataa huyo X-something wako, uilinde ndoa yako.

Yani unataka uwe na waume wawili au?? Manake mwanaume huyo unamwamini je kama nia yake ni nzuri,
kwenye hiyo ndoa yako. Mijitu mingine wakati mwingine inadhamiria kukuharibia maisha milele wewe dada!!
Acha huruma ya kijinga wewe. Usije mlaumu Mungu bure. Amekupigania kote huko unataka uharibu tena.

Think!!!!! Mwambie ukukome, wakati utaamua mambo, kwanza akafight huko alete matunzo ya mtoto kama anataka mtoto!!

Yaani hata kama huyo mwanaume ni baba yangu, nita mdefine hivi hivi!!
 
Achan nae kabisa badili na namba ya simu huyo ni anatumiwa na shetani tu aje kukuangamiza, mume wako akigundua inavyowasiliana nae doa lake utalitibu miaka nenda rudi hatakuamini tena kwa chochote kile. kaa nae mbali mwambie muda wake aliuchezea sasa umeolewa hutaki usumbufu. ukiona anazidi muite mahala akija unakuwa ushamwambia na mumeo nae anakuja then mnamuuliza tatizo lake ni nini? nikwambie kitu! wanaume wengine wanapenda mkiachana akuone unadondoka kwa kila kitu, watch out mydia.
 
alimpa namba yake ya simu ya nini naye???...kama alimuacha siku nyingi na hakutaka kujua lolote kuhusu yeye means hakuwa hata na contact naye...au ametafuta mawasiliano kutoka kwa rafiki zake? kama ni hivyo hawakumueleza sasa kama ameolewa?...mnh

Huyo dada naona anachezea shillingi kwenye tundu la choo.
Amweleze mume wake kila kinachoendelea na awe wazi, abadili #, na akome kabisa kuwasiliana na ex wake sababu sio fair kwa mumewe.
Kama ingekuwa ni ughaibuni huyo ex- angepigwa restraining order na asingethubutu kumpigia simu huyo dada, na akijaribu tu basi jela kunamsubiri kwani atakuwa amecommit communication threats/violation of restraining order.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…