Dada huyu anaomba Msaada wenu kimawazo .....


Hayo ndo matatizo ya stori za kutunga. Unajiua kutokuwa na mahusiano wa miaka 6 si mchezo. Haiwezekani kuwa huyo mume aliyefunga naye ndoa halijui suala hilo kwa kluwa mtoto wa jamaa si anamfahamu. Haiwezekani jamaa wa zamani afosi king namna hiyo kama hakuna kingine zaidi ya hivyo ulivyoandika hapo. Ushauri: Cha msingi huyo dada amshitaki huyo jamaa kwa kumbugudhi katika maisha yake
 
Huyu dada na amweeze ukweli huyo mwanaume kuwa yeye hana mpango naye na asimharibie maisha yake kwani wakati alivyokuwa amemtelekeza alizania ndo amefika.Ampige marufuku kumtumia hizo meseji asije akamharibia ndoa yake bure
 

Ni kweli hili tukio lipo Lutala na si la kutunga ,
Story itungwe ili iweje shemeji??
 
wanawake bwana!!!!!!!!!!!!!! hilo nalo linahitaji ushauri jamani. kama ndoa yake haipendi ndo aombe ushauri. ila kama anaipenda ndoa yake basi jibu analo mwenyewe.
 
Huyu mdada amwambie mumewe ili from there wajue wanaanzia wapi, kabla jahaz halijazama. Wanaume bana aaah!
 

kwangu mimi best yako yu week na ampenda huyo wa zamani. alipa namba ya nini!? na anakuwa nae karibu ki vipi mtu alimtosa hadi mtoto? au anatuongopea kama hakuwahi tunzwa? mwambie yuko week ajaribu kuwa strong ataachwa.
 
Hana sababu hata ya kupokea simu yake, na aachane naye mara moja! Huu wema wa namna hiyo ulishaponza wengi! Amwambie samahani sitaweza kukusaidia, basi -tena kwa message/sms na kisha ai-ban hiyo namba!!!! Asiposikia haya, akiachwa aje atuarifu!
 
Huyu dada na amweeze ukweli huyo mwanaume kuwa yeye hana mpango naye na asimharibie maisha yake kwani wakati alivyokuwa amemtelekeza alizania ndo amefika.Ampige marufuku kumtumia hizo meseji asije akamharibia ndoa yake bure
Shida yake yeye si kurudiana,bali anaomba ampe mtaji ili umsaidie kuanzisha biashara!!
 
wanawake bwana!!!!!!!!!!!!!! hilo nalo linahitaji ushauri jamani. kama ndoa yake haipendi ndo aombe ushauri. ila kama anaipenda ndoa yake basi jibu analo mwenyewe.

Mkuu yeye anaomba msaada namna na kuepukana na bwana wake wa zamani!
 
Mimi nafikiri akamshitaki kwenye balaza la wazee,na awe wazi kabisa kwa mume wake wa ndoa!wazee wenye busara watalipatia ufumbuzi!!
 
Mi navyoona huyo mwanamme anataka kuharibu tu ndoa ya mwenzie, kwani haweze kuomba pesa sehemu nyingine? Haf huyo mwanamke asilee ujinga, amwambie kabisa haiwezekani tena kuwa na uhusiano wa karibu.
 
kwa nini asinunue line mpya? hivi kubadirisha line ni kiasi gani?
pile, ampe taarifa mwenzi wake ili aelewe
ila afanye kwanza la kwanza na akiona limefeli basi aende la pili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…