Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
Rose Kimaro mkazi wa kijiji cha Otaruni Kibosho kati wilaya ya Moshi ambaye ni dada wa Getruda Shio anayedai kuwa alipigwa makofi na mkuu wa wilaya ya Moshi, James Kaji ofsisini kwake, ameibuka na kueleza kisa chote na kukana mkuu huyo wa wilaya kumpiga makofi mdogo wake.
Rose emeenda mbali baada ya kufichukua kuwa,mdogo wake huyo anachangamoto ya afya ya akili kwani akiwa na umri wa miezi tisa alipigwa kichwani na Baba yake mzazi wakati wa ugomvi na mama yao na kupelekwa kwenye matibabu katika Hospital ya Mkoa, Mawenzi kwa ajili ya matibabu.
Mama huyo mwenye umri unaokadiriwa kuwa na miaka 57,amezungumza na waandishi wa habari leo mjini moshi na kuelezea namna sakata hilo lilivyo baaada ya kuibuka kwa taarifa za Mkuu huyo wa wilaya kudaiwa kumpiga makofi mwananchi huyo ofisini kwake.
"Niseme tu kutoka rohoni ,huyo baba mkuu wa wilaya alitoa rozali akawambia kwa haya mnayoyafanya huko kwenye ukoo wenu kumkandamiza huyu mama ipo siku mungu atawaumbua",alisema rose ambaye ni mama wa watoto sita.
Mama huyo ambaye katika siku za hivi karibuni alikamatwa na polisi na kushikiliwa kwa siku 24 akihusishwa na kifo cha mama yake mzazi,Anastazia Shio(87),amedai kuwa mdogo wake alikaidi magizo ya mkuu wa wilaya aliyemtaka kuwasilisha kwake hati ya kifo cha mama yao mzazi hadi hapo mgogoro huo wa kifamilia utakapopatiwa ufumbuzi.
Pia, soma: Mwananchi Arusha adai ametukanwa na kuchapwa makofi na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, DC asema "aende Mahakamani"
Anasema mkuu huyo wa wilaya alitumia kila aina ya busara kumtaka Getruda kuikabidhi hati hiyo kwa mkuu wa wilaya lakini mdogo wake alisisitiza hawezi kufanya hivyo huku akionyesha kuwa na ghadhabu hali iliyompelekea mkuu huyo wa wilaya kumwagiza katibu tawala wake,Shaaban Mchomvu kuwasiliana na mkuu wa polisi wa wilaya.
Anasema muda mfupi OCD alifika ofisini kwa mkuu wa wilaya akiwa ameambatana na askari wa kike na wakamchukua hadi kituo kikuu cha polisi ambako hata hivyo aliachiliwa muda mfupi baada ya kukabidhi hati hiyo.
Mbali na hilo,mama huyo naye aliongozana na askari hao hadi kituo kikuu cha polisi ambako alifungua jalada la uchunguzi kutokana na kuwepo kwa vitisho kutoka kwa watu aliodai wanatoka upande wa pili wanaodaiwa kuchochea mgogoro huo.
AKANA KUHUSIKA NA KIFO CHA MAMA YAKE
Mwezi Agosti mwaka huu Rose alikamatwa na kusota mahabusu ya polisi kwa siku 24 akidawa kuwa alimuua mama yake Mzazi Anastazia Shio na kudaiwa kutaka kumzika chap chap na baadae kufikishwa mahakamani ambako alisomewa shitaka la kuua bila kukusudia.
Rose ameelezea kwa kirefu sakata hilo akidai linchangiwa na watu wanaotaka shamba lililoachwa na mama yake ambao anadai wanafanya hivyo ili kutimiza matakwa yao ya kuliuza bila wanufaika wengine kunufaika na shamba hilo.
Anasema Agosti 13 alipigiwa simu akitaarifiwa mama yake anaumwa na akatakiwa kwenda kumchukua ili ampeleke kwenye matibabu na alifanya hivyo lakini mungu alimchukua siku hiyo hiyo usiku wa saaa nne na nusu.
Anasema mara baada ya mama yake kufariki aliwajulisha ndugu zake na kuanza kuandaa tararibu za mazishi lakini shughuli za mazishi zilisitishwa na vyombo vya dola baada ya kuelezwa kuwa kifo cha mama yake kina utata.
"Tuliandaa shughuli za mazishi wa siku tano,wakati tunaandaa mazishi ndugu zangu walikuwa wanaendelea na vikao vya kunitengenezea mazingira ya kunifungulia kesi ya mauaji ya mama yangu na nilipoenda chumba cha kuhifadhi maiti kwa lengo la kulipia gharama za kuhifadhi mwili wa mama yangu tayari kwa ajili ya mazishi,niliambiwa niende polisi".
Anasema wahudumu wa chumba cha kuhifadhi maiti walimweleza kuwa polisi wanadai kuna tetezi kuwa kifo cha mama yake kina mashaka na alipoenda polisi alikutana na mkuu wa upelelezi wa wilaya(OC-CID)ambaye alihoji ni kwa nini anataka kwenda kumzika mama yake bila kushirikisha ndugu zake na licha ya kujitetea bado OC-CID alimweleza kuwa yeye(Rose)ndiyo aliyehusika na kifo cha mama yake.
Mwili huo ulihamishwa kutoka mawenzi na kupelekwa Hospital ya Rufaa ya Kanda ya KCMC ambako ulifanyiwa uchunguzi na kubainika kuwa marehemu alikuwa amevunjika mbavu nane na kwa mujibu wa Rose upande mmoja ulibainika mbavu tano zilikuwa zimevunjika na upande mwingine mbavu tatu.
Mbali na mbavu,Rose anasema pia ilibainika pafu lake moja la upande wa kulia lilikuwa limeharibika na akahitimisha kwa kueleza kuwa mama yake alikuwa anatumia ugoro na pengine inaweza kuwa moja ya sababu iliyochangia kuharibika kwa mapafu yake.
MWISHO
Pichani kulia ni Rose Kimaro aliwa na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa ukoo wa Shio, Frances Shio kushoto.