Dada wa kazi anajua ratiba zangu kuliko Mke wangu!

Daaaahhhh yaani mtu anaonyesha bidii na kujituma kwenye kazi yake ili apate rizki yake halafu wewe unashauri amuondoe(amfukuze) kazi ni haki kweli?
Unajua katika huo mshahara anaoupata kuna watu wangapi nyuma yake wanamtegemea?
Hapo kwa ushauri wangu ni bora amuongezee mshahara ili kumpa molari zaidi kwenye kazi na kumfanya aone jitihada yake inathaminiwa.
 
Ni maamuzi yake pia. Ana uhuru wa kuchagua
 
Hajui kuwa kuna housegirls wanakuja nyumba za watu kuvuruga tu ndoa kujifanya wanajua caring kumbe wanawinda.....bora tu afukuze mapema kabla ya kufikwa na aibu.
 
Ulivyosema pia inawezekana ni kujituma ila
na vp km kaja kwa malengo yake binafsi? Labda tujue kabila gani huyo msichana kwanza.
 
Huna lolote mwaisa we sema umemcrushia bekitatu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ndio maana akawa dada wa kazi..hayo ni majukumu yake!
 
Kuna mwanasaikolojia mmoja alisema kila mwanaume anatafsiri yake kuhusu kuheshimiwa na kupendwa na mwanamke..unajua jambo hilo hadi umeleta hapa means limekugusa sana hadi ndani ya moyo wako...kitendo cha kufanyiwa jambo na mwanamke(house girl) bila kumwambia ni jambo lilokuvutia na kuona ni kitu unahitaji kifanyike ...huyo housegirl akiongeza kasi tu kidogo basi atauteka moyo wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…