Hili lidada nilijinga , bado linaongelea athari za ukolon hadi leo!
Hadi sasa Africa ndiyo inalialia kuhusu ukolon na athali zake. mabara mengine walishasahau na kumove on.
Achen kujidanganya, ruhusun viongozi na waongozwaji wenye akili waitawale Africa sio nyinyi.
Unakashifu lakini ukweli ni kwamba hii mada imekupita sana kimo. Walau ungekuwa unafahamu historia ya dunia, mifumo ya biashara, sheria za kimataifa na muingiliano wa watu, basi ungekuwa makini sana kwenye kutoa hoja. Huenda hata ungenyamaza na kuwa muungwana: Hebu nikuthibitishie tu hili nalozungumza hapa, nikiwianisha na hoja ulizozitoa:
Mosi, unasema hadi sasa Afrika ndiyo inalia kuhusu ukoloni na athari zake, mabara mengine walisahau na kuendelea mbele: Huu ni ufinyu mkubwa sana wa mawazo (Parochialism) ambao sikutegemea kuuona kwa msomi wa Afrika tena wa kizazi hiki. Hebu tuanze na bara la Marekani ambako watu kama wewe huenda hawafahamu kinachoendelea.
1. BARA LA AMERIKA KASKAZINI (NORTH-AMERICA)
Marekani aliua maelfu ya wahindi wekundu na mpaka leo amewekea sheria za kuwalipa fidia maalumu. Mwaka 1946 aliunda tume maalumu (Indians Claims Commission) ambayo ilifanya uchunguzi kwa waathirika ambao walilipwa zaidi ya bilioni 1.3. Kumbuka mauaji ya wahindi wekundu katika sehemu kubwa yalifanyika miaka zaidi ya mia tatu iliyopita hata kabla ya Marekani halijawa taifa. Nini kilipelekea hili jambo la kudai fidia miaka zaidi ya mia moja baada ya tukio lenyewe kufanyika ??? Utasemaje ni Afrika peke yake wanaokumbuka mambo ya zamani ???
Upande mwingine harakati za The Black Lives Matter Movement (BLM) ambazo zimekuwa zikiendelea nchini Marekani chanzo chake kikubwa ni nini haswa ??? Kipi kinapelekea wanaharakati wa mlengo wa kushoto (Weusi, Wazungu, Latino) kuvunja masanamu ya mashujaa wengi wa Marekani hasa wa majimbo ya kusini, ambayo yalitengenezwa kipindi cha Karne za 18 na 19 ??? Hili linafanyika barani Afrika ???
Chanzo:
Photos: The Statues Brought Down Since the George Floyd Protests Began
Mwaka huu siasa za nchini Canada zimetiwa doa na zimwi la Ukoloni baada ya kapatikana kaburi la pamoja (Mass Grave) la watoto wa wahindi wekundu zaidi ya 1000 chini ya shule ambayo ilikuwa inamilikiwa na kanisa. Jambo hili la kikoloni na kibaguzi, lilifanyika zaidi miaka ya 1800's huko, ila limezua hisia kali sana kwa wananchi wa Canada na mpaka sasa ni mjadala wa kitaifa ambao utawatesa mawaziri wakuu wengi wajao pamoja na kuligawanya taifa. Hebu nikuulize hili linafanyika Afrika ???
Chanzo:
How Thousands of Indigenous Children Vanished in Canada
2. BARA LA AMERIKA KUSINI (SOUTH-AMERICA)
Mpaka mwaka huu waziri mkuu wa Barbados Mia Motley akihojiwa na BBC amesema kwamba nchi yake inajitoa kwenye nchi wanachama wa Jumuiya za Madola na kumfanya Malkia asiwe mkuu wa nchi ili kufutilia kabisa historia ya Ukoloni nchini humo. Lakini pia kasema wataendelea kudai fidia kwa biashara ya utumwa ambayo ilifanyika kwenye nchi hiyo zaidi ya miaka 500 iliyopita.
Chanzo hiki hapa angalia mwenyewe:
Moja ya jarida la Uingereza linaloheshimika duniani kwa kufanya tafiti nyingi za kisayansi
The Financial Times limezungumzia hili suala la ukoloni na nchi za duniani na jinsi gani ambavyo madai haya yanawanyima raha mabepari wa Ulaya. Kukupasha tu habari, jarida hili limekiri kwamba mafaniko mengi ya Ulaya mpaka leo hii yamechangiwa na ukoloni na biashara ya utumwa.
Kuna familia ambazo zilikuwa zinajihusisha na biashara ya watumwa, zilipata hasara zaidi ya miaka 500 iliyopita kwenye meli zao za watumwa. Wakaidai serikali ya Uingereza fidia na kuacha madeni ambayo vitukuu vyao vimeyarithi. Unajua hayo madeni ya kufidia familia za wauza watumwa yamemalizwa mwaka gani ??? Mwaka 2015.
Lakini wewe mmatumbwi hustuki na unaona hili ni sawa kabisa kichwani mwako. Kibaya zaidi umekuja hapa kukebehi na kukashifu watu: CCM ni tatizo, lakini siyo tatizo kubwa kama wasomi wa aina yako.
Hebu pitia chanzo hiki:
Subscribe to read | Financial Times
3. BARA LA ASIA (ASIA)
Hivi unafahamu kwamba hitilifu kubwa za kiusalama kule barani Asia zinachangiwa na ukoloni au hutafahamu hili ??? Tena heri sisi Afrika tunazungumza tu, wenzetu hawa wanatumia hadi silaha za moto kupambana. Hebu nikupe mifano:
Mosi, chanzo kikubwa cha mgogoro wa Israeli na Palestina ni ukoloni: Muingereza, Mfaransa na Machifu wa Kiarabu ndiyo waliosaini mikataba ambayo imeliweka lile eneo lote rehani. Mikataba imesainiwa hata kabla ya Palestina na Israeli kuwa nchi. Unakumbuka The Balfour Declaration 1917 na Mkataba wa Sykes-Picot 1916 ??? Huwezi kujadili mgogoro wa Palestina na Israeli bila kuweka suala zima la Ukoloni mezani. Wewe mwenzangu unaonaje labda ???
Pili, kukupasha habari zaidi. Mwaka huu 2021, mahakama ya Korea Kusini imetoa amri kuitaka serikali ya Japan kuwalipa fidia wanawake wa Kikorea ambao walifanyiwa vitendo vya kinyama na serikali ya kikoloni ya Japan kipindi cha vita ya pili ya dunia. Kila muhanga/muathirika au familia yake wanatakiwa kulipwa dola za kimarekani 91,000 ambazo ni kama milioni mia mbili za kitanzania.
Korea-Kusini ni nchi iliyoendelea kuliko nchi yoyote ile ya Afrika, lakini wasomi wake ambao wana elimu bora kuliko wewe na mimi wanayona madhara ya ukoloni hadi leo.Ila wewe ndugu yangu uliyesoma UDSM, UDOM, MZUMBE au KAMPALA huoni matatizo yaliyoletwa na ukoloni barani Afrika. Wewe unahisi kila kitu kimesababishwa na CCM na kinaweza tatuliwa na CHADEMA. Kama unawaza hivi basi utachelewa sana kufika rafiki yangu, utachelewa mnooo.
Chanzo:
South Korea ‘Comfort Women’ Compensation Verdict Angers Japan
Tatu, natumai umeziona vurugu zilizotokea Hong-Kong mwaka huu. Hivi unafahamu chanzo chake haswa ni nini ??? Sikutaka kukujibu, lakini kwasababu umesema kabisa hili tatizo la ukoloni liko Afrika peke yale, basi naomba nikufumbue macho. Uchina alirudishiwa Hong-Kong kutoka Uingereza mwaka 1996 tokea mwaka 1842. Mpaka leo Uchina anasumbuliwa na masharti ya mkataba wa Kikoloni ambao alisaini na Muingereza ili Hong-Kong irudishwe mwaka 1996.
Lakini, kikubwa ambacho unatakiwa ukifahamu ni hiki: Uchina ni taifa kubwa sana, lakini siku ambayo Hong-Kong inarudishwa Waziri Mkuu wa Uingereza John Major alitoa hotuba kwamba "Yaliyopita si ndwele tugange yajayo" lakini Raisi wa Uchina Jiang Zemin akamkemea na kusema "Hatuwezi kujifanya tunasahau na kufumbia macho madhara ambayo utawala wa waingereza umeleta nchini Uchina "
Huyu ni Raisi wa taifa kubwa na kongwe zaidi duniani, aliyasema haya mwaka 1996, lakini wewe mmatumbwi wa nanjilinji unahisi kabisa kwamba ukoloni haujaacha madhara barani Afrika. Kama madhara ya ukoloni, ubaguzi na utumwa yanaonekana kwa nchi kubwa na tajiri kama Uchina, Marekani, Canada na Korea-Kusini, sisi nchi masikini za Afrika unahisi kabisa tunaweza kwenda mbele bila kufanya tathmini yakinifu kuhusu madhara ya ukoloni ???
4. NAMALIZIA BARA LA AFRIKA
Mtu yoyote ambaye walau ameenda shule vizuri na anatumia kichwa chake kufikiri na siyo tu kufuga nywele, ndevu na kuvaa rozari au baraghashee lazima atang'amua kwamba katika sehemu zote ambazo ukoloni umeacha madhara makubwa basi ni barani Afrika. Hebu sasa nihitimishe kwa kukwambia wewe na wenzako wa aina yako ni kwanini:
Tofauti na sehemu nyingine kama Asia ambako wakoloni walikuta mataifa makubwa ambayo tayari yalishaendelea (Advanced Civilizations), huku Afrika mataifa makubwa yalikuwa machache sana. Hivyo walichofanya ni kuchora upya mipaka yao kule Berlini mwaka 1885 bila kuhusisha waafrika na kuwaweka watu ambao hawahusiani kwa lolote lile ndani ya koloni moja. Kibaya zaidi wanavyoondoka walituachia mipaka yao ile ile. Mpaka leo asilimia 80% ya migogoro mikubwa barani Afrika inachangiwa na mipaka ya kikoloni.
Mosi, ugomvi wa Tanzania-Malawi dhidi ya ziwa Nyasa/Malawi umesababishwa na mkataba wa kikoloni wa Heligoland wa mwaka 1890. Mkataba huu ulisainiwa na Muingereza, Mjerumani na Sultani wa Zanzibar kuhusu kugawana maeneo, mojawapo likiwa ziwa nyasa. Mpaka leo hii huu mkataba unatubana watanzania/wamalawi na kutatokea taharuki hivi karibuni endepo hatutakubaliana juu ya hili.
Leo hii ziwa akipewa Malawi ina maana wilaya nne za Tanzania : Mbinga, Ludewa, Nyasa na Kyela zenye wakazi zaidi ya 1,000,000 ambao hutegemea ziwa kwa shughuli zao za kimaisha wataumizwa. Sijui kama hata ubongo wako unang'amua hiki nachokisema hapa. Hata wewe na wenzako mnaopiga ngenga mkidhani kila kitu ni CCM mtaathirika nakwambia. Likitokea lolote kule dhidi ya Tanzania basi tegemea vita, tena vita kubwa tu. Colonialists left us in this predicament: YOU CAN TAKE THIS TO THE BANK.
Pili, ugomvi mkubwa wa Cameroon-Nigeria juu ya rasi ya Bakassi (Bakassi Peninsula) ambao mpaka leo umeondoa maisha ya watu wengi umesababishwa na wakoloni wa Kiingereza na Kifaransa ambao walitawala hizi nchi mbili. Wao walisainishana mikataba mwaka 1913 huko lakini mpaka leo unaleta matatizo barani Afrika. Lile eneo mahakama ya kimataifa (International Court of Justice) imempa Cameroon.
Lakini maelfu ya wanaijeria wamekuwa wakiishi pale kwa miaka zaidi ya 100. Leo hii unawaambia wachague uraia wa Cameroon na wakishindwa warudi Nigeria: Hivi huku siyo kutengeneza vita kweli ??? Nini kimesababisha haya kama siyo UKOLONI.
Tatu, kukupasha tu kuna barani Afrika kuna migogoro zaidi ya 100 kuhusu mipaka iliyoachwa na wakoloni ambayo inaweza kuleta taharuki siku za mbeleni, hasahasa ambapo ugunduzi wa madini na mafuta unafanyika kwenye hayo maeneo. Nashangaa sana kuona msomi unakuwa huyafahamu kabisa haya. Hapa utatakaje tusonge mbele bila kuzungumza madhara ambayo ukoloni unaendelea kufanya dhidi yetu ???
Ningezumguzia na kukuonesha jinsi mifumo ya sheria za dunia za kiuchumi, kibiashara, kidiplomasia na kiulinzi ambavyo ina mizizi mizito ya kikoloni na inaziumiza nchi za Afrika hadi leo hii, ila nina uhakika hatutaelewana kabisa kama tu mambo madogo aliyoyasema huyo dada wa kikenya umeshindwa kuyaelewa.
NB 1: Niseme ukweli, huyo dada unayemkebehi wewe amekushinda kila kitu. Nina uhakika asilimia 1,000,000,000,000,000% wewe huwezi kusimama mbele za watu na kuzungumza lugha ya kiingereza kwa ufasaha kwa kiwango hicho. Lakini nina uhakika tena kwamba huwezi kusimama mbele hata ya darasa la watu 50 na kuzungumza kwa ufasaha hata tukikuruhusu kuzungumza mada ya KIPUMBAVU.
NB 2: Ungesikiliza hadi mwisho majibu ya Raisi wa Ufaransa jinsi alivyomjibu huyo dada nadhani ungeelewa vizuri kabisa. Emmanuel Macron na wageni wote walimuelewa huyo dada lakini wewe Mmatumbwi hujamuelewa. Aidha wakina Macron na wengine ndiyo wajinga, AU wewe mmatumbwi ndiyo hujaelewa.
NB 3: Hawa hapa waandishi nguli kutoka Afrika (Wole Soyinka-ambaye amewahi kupata tuzo ya Nobel ya Literature ) na Chimamanda wanazumzia madhara ya ukoloni barani Afrika. Hawajazungumza tofauti sana na huyo dada. Lakini wewe jamaa yangu nadhani uko na akili kupita kiasi..
-CHIMAMANDA ON COLONIALISM
-SOYINKA ON RELIGION AS AGENCY FOR IMPERIALISM
NB 4: Halafu WIN TO WIN CONTRACTS ndiyo Contracts zipi hizo ??? (Bwahahahaha) 🤣 🤣 🤣
Like Notorious B.I.G once said in his infamous Juicy, "
If you don't know, now you know Nigger"