Dada yangu anavimba mwili, msaada

Joined
Aug 10, 2013
Posts
76
Reaction score
7
Huwa anatokewa na uvimbe mwilini alafu yanavimba yanakua mekundu kama mtu aliyeumwa na mende yanamuuma sana jamani, msaada.
 
hua anatokewa na uvimbe mwilini alaf ya navimba yanakua mekundu kama mtu aliyeumwa na mende yanamuuma sana jaman msaada

Sasa wewe badala ya kumpeleka kwanza hospitali unataka ushauri wa watu humu ndani? Ninakupa huduma ya kwanza kesho mpeleke hospitali.

Chukuwa asali kijiko kimoja na changanya na mdalasini kijiko 1 weka katika maji ya uvuguvugu glasi 1 mpe anywe mgonjwa kutwa mara 3 atapungukiwa kuvimba mwilini.

Kuvimba Mwili kunasababishwa na mojawapo kati ya haya hapa chini:

1. shinikizo la damu la ujauzito (pre-eclampsia).

2. magonjwa ya figo - hii mtu huvimba, pamoja na miguu, uso pia.

3. magojwa ya ini - haya husababisha pia maji kujaa kwenye ukuta wa mbele wa tumbo (ascites) lakini pia mwili wote waweza kuvimba

4. Ukosefu wa protein kwenye damu (hypoproteinaemia kwa sababu yoyote).

5. Ugonjwa wa moyo (heart failure) n.k.

Ni vizuri mama anapovimba miguu aende hospitali kwa ajili ya uchunguzi, atatibiwa kulingana na tatizo litakalogundulika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…