Dada yetu ameolewa na tajiri lakini hataki kumuibia mume wake hela ili atukwamue na sisi

Duh Bob marley aliwahi kuulizwa wewe ni tajiri?

Jibu alilotoa mpaka leo naishi nalo!
 
MWAYA MWAMBA CHUKUENI CHENU MAPEMA IKITOKEA JAMAA KAZIMA NDUGU WAKAMTIMUA DADA YENU, MTAJUTIA HIZI SHOT OFF TARGET MLIZO KOSA,
 
Mada za kingese kama hizi afu tukicomment KAMSEMEE KWA BABAAKE mnakuja na mada kutusema hatuna akili
 
Ulivyo jinga ningemshauri dada yako akuwekeee sumu siku ukimtembelea apunguze mbegu mbaya duniani
 
Inaweza ikawa ni stori tu ya kufurahisha genge, ila kikukweli mabinti wengi kutoka familia za kimaskini wanaoolewa na matajiri ndugu zao huwa wana akili za namna hii.

Kwanza wanakuwaga very entitled na pesa za mkwe wao, maana wakiona binti yao ameshindwa kutumia pesa za mume wake kuwanufaisha wao wanamlaumu sana.

Na endapo kama binti yao akiwa ni kichwa maji huwa wanaenda mbali na kumshauri amuue mume wake hili arithi mali kuunufaisha ukoo wao mzima bila kelele.

Hapo ndipo huwa naelewa kwanini mtoto wa ASAS utakuta anaoa mtoto wa OILCOM na wala huwezi kukuta anaenda kuoa binti aliyekulia huko Mburahati, kuna mengi wanayeupuka.
 
Na wewe mtafute GSM akuoe uwe na maisha usaidie ndugu zako waliobaki bush
 
Naona wanaJF wamekupatia ulichokua unakitafuta.
 
Mnataka aachike, arudi kijinini mteseke wote,

Ungekuwa na akili, ungesema awatafutie kazi kwa shemeji yenu hata ya kuendesha magari ila mnakazania aibe,

Shenzi kabisa
 
Huna hata aibu kuja hapa kujitangazia kuwa wewe na mama yako hamna uungwana na mna tabia za wizi? Kama mnashida ni kwa nini hamumuombi shemegi yenu akusaidieni? Amemuona dada yenu kwa hivyo ameunga ukoo na nyie sasa ni kwa nini mnataka kumuibia? mlijaribu kumuomba msaada akakataa? mnata dada yenu amuibie mumewe? are you for real? Come on una miaka 31 na unashindwa kutafuta njia za kujitatua kimaisha unataka mdogo wako aibe kwa manufaa yako?! Kama kweli unataka kujitatua kimaisha si uende tu kwa shemegi yako umuelezo matatizo yako umuombe ajira, ushauri au mkopo? Hivi umefikiri itakuwaje kama mdogo wako akiamua kumuibia mumewe na akagundulikana na kuachwa utafanya nini? Utaweza kumtunza mdogo wako wakati wewe mwenyewe kwa umri huo ulionao huna idea ya vipi kupambana na maisha bila ya kuiba?
 
Sababu ya umasikini wako ni kutokuwa na akili, unatamanije mtu aibe kitu cha mwenzie? Hiyo ni dhambi katafute chako, kwanini usiombe? Au mnataka familia nzima muolewe na huyo shemeji yenu ili mpate hela?
 
aina hii ya familia hapa bongo ni nyingi na hata wakipewa pesa hawawez kuziendeleza na mwisho mabinti wengi wameshindwa kulinda ndoa zao kwa upuuzi km huu yani kiufupi familia ya mleta uzi ni vichwa maji ispokuw huyo dada alieolewa na tajiri
lakn pia ukute hata huyo dada nae ni kibaka tu ila kabanwa na mifumo so asipate urahisi wa kudokoa pesa🥺
 
Mada kama hizi kule Facebook zimejaa kuchangamsha genge na kuwaliwaza watanganyika.

Replies nyingi huwa ni comedy 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…