Dada yetu anaishi na Virusi vya UKIMWI, tumwambie ukweli mchumba wake?


Ndugu yangu kiuhalisia wa tatizo lilivyo wewe haupaswi kumwambia shemeji yako chochote kile mwenye mamlaka ya kumwambia ni dada yako. Jukumu lako wewe ni kumshauri dada yako ili aweke wazi. Ukimweleza shemeji yako chochote kile dada yako anaweza kukushtaki na ukachukuliwa hatua za kisheria.
 

mabadiliko ndo yataletwa na watu wanaofikiria nje ya boksi. Hii nchi hatuendelei kwa sababu hatuchukui hatua kwenye mambo tunayodhani hayatuhusu. Ndo maana tunazungukwa na taka na maji machafu kwenye mitaro inayopita nje ya nyumba zetu kwa sababu tunaona ni kazi ya serikali, ndo maana tunaacha watoto wa majirani zetu wanateseka au wake zao au waume zao haturipoti polisi au ustawi wa jamii kwa sababu tunaogopa kugombana na jirani! Ndo maana hatuzimi taa na ac maofisini kwa sababu si za nyumbani kwetu....... Akiongezeka mwathirika mmoja wa VVU tunaongezea taifa mzigo wa kumhudumia maana arv hazilipiwi na mgonjwa. tukiacha wazazi watarajiwa wakaambukizana VVU na wakazaa watoto wenye VVU tunarudi pale niliposema mwanzo. Wakizaa watoto wasio na VVU - shukrani kwa teknolojia, kuna siku wataachwa yatima. Nani atawalea? Mjomba? Serikali? Mitaa? watu wanao-mind their own business? na kwa social security ipi iliyopo tanzania? Bila kusahau muda tunaopoteza kuuguza wagonjwa badala ya kwenda kuzalisha ili tupate maendeleo, achilia mbali gharama tunazoingia kuuguza wagonjwa badala ya kutumia fedha hizo kusomeshea watoto au kujiwekea akiba au kuchangia miradi ya maendeleo.

afu kusema shemeji hata asipokufa kwa ukimwi atakufa anyway...ni mawazo yanayoturudisha nyuma kimaendeleo kabisaaaaa....ni sawa na kusema tusipige vita ajali za barabarani, tusipige vita kansa, tusipige vita vifo vya kinamama wazazi na watoto under 5, tusipige vita maambukizi mapya ya vvu n.k kwa sababu watu watakufa anyway!!
 
kama dada amekataa je? na unaweza kutaja japo hatua moja tu kisheria ambayo dada anaweza kumchukulia kaka yake?
 

Da Asia, upo sahihi kabisa but itachukua miaka mingi sana watanzania kuujua UKIMWI, na hapa ndiyo turning point ya vifo vingi vya watu wenye HIV. Kuna watu huwa wanaweka mada humu kuhusu mwafrika kuwa na akili ndogo. Ukweli ni kwamba watanzania tulio wengi sio wafatiliaji wa mambo, sio wasomaji, huu ugonjwa wa UKIMWI hauwezi kumpata tu kila mtu na ni ugonjwa wa kawaida sanaaa but ni vigumu kupindua nadharia iliyoaminika kwa miaka zaidi ya 30 kwamba HIV=AIDS=DEATH. Na nasikitika kusema kwamba watanzania na waafrika kwa ujumla tumeamua kutotaka kuujua ukweli wa huu ugonjwa, watanzania kuanzia mwaka 1984 mpka leo 2015 bado wanaamini UKIMWI umeletwa na mungu kama adhabu, huu ni kukosa maarifa kwa kiwango cha juu sana. Anyway acha tufe kwasababu ya kulack knowledge.
 
Sasa jamaa hajapiga mfulele wa dada yako tena bila ndom? Na alivoona mfulele mtamu ndio akaanza harakati za kutoa mahali
 
Hapo Kuna Mengi.
>Inawezekana Jamaa Nae Anao Na Anajua Binti Hana Na Hajamwambia.
>Au Wanaweza Kuwa Pmj Na Jamaa Asipate Ukimwi, Kwa Sbb Neno Linasewa Roho Itendayo Dhambi Ndiyo Itakayokufa.

>Lakini Pia Cjajua Kama Kijana Alimshirikisha Mchungaji Wake Kuhusu Huyo Binti? Maana Hayo Ndiyo Madhara Ya Kukutana Vichochoroni Alafu Ndoa Ikifika Ndo Mnakimbilia Kwa Mchungaji.

Lakini Ninyi Pia Mnashiriki Dhambi Pmj Na Dada Yako Kwa Kukaa Kimya, Cha Msingi Hapo, Wewe Unaweza Kwenda Kwa Mchungaji Kutoa Taarifa Bila Wao Kujua Hata Kama Wewe Hauabudu Hapo.

Lakini Pia Kama Yupo Vzr Kiroho, Inawezekana Mungu Anataka Kumfanyia Muujiza Wa Kumponya Ukimwi Huyo Dada Cku Ya Ndoa.

Kwa Ushauri Zaidi Tuwasiliane. By Pastor Emmanuel: 0757856336,au 0673100772
 
Hapo Kuna Mengi.
>Inawezekana Jamaa Nae Anao Na Anajua Binti Hana Na Hajamwambia.
>Au Wanaweza Kuwa Pmj Na Jamaa Asipate Ukimwi, Kwa Sbb Neno Linasewa Roho Itendayo Dhambi Ndiyo Itakayokufa.

>Lakini Pia Cjajua Kama Kijana Alimshirikisha Mchungaji Wake Kuhusu Huyo Binti? Maana Hayo Ndiyo Madhara Ya Kukutana Vichochoroni Alafu Ndoa Ikifika Ndo Mnakimbilia Kwa Mchungaji.

Lakini Ninyi Pia Mnashiriki Dhambi Pmj Na Dada Yako Kwa Kukaa Kimya, Cha Msingi Hapo, Wewe Unaweza Kwenda Kwa Mchungaji Kutoa Taarifa Bila Wao Kujua Hata Kama Wewe Hauabudu Hapo.

Lakini Pia Kama Yupo Vzr Kiroho, Inawezekana Mungu Anataka Kumfanyia Muujiza Wa Kumponya Ukimwi Huyo Dada Cku Ya Ndoa.

Kwa Ushauri Zaidi Tuwasiliane. By Pastor Emmanuel: 0757856336,au 0673100772
 
kama dada amekataa je? na unaweza kutaja japo hatua moja tu kisheria ambayo dada anaweza kumchukulia kaka yake?

Kuna nchi zinataka kutunga sheria dhidi ya watu wanaoambukiza wengine ukimwi kwa makusudi.
 
Waacheni hamuwezi jua wote wawili wakoje,kama jamaa angekuwa anajali si angemwambia wakapime?hiyo shemeji nae ni wale wale tu acha waungane wawe kitu kimoja.
 
Mngemshauri shemeji wakapime, mwambieni kama mnamuuliza hivi kama wamepima.
 
Duh..ni miaka sasa hatujawa na harusi tunachangia (in my mama voice) hahahahaha
 
Watanzania si wasomaji wazuri, tunakurupuka ndio maana tuko ignorant kwenye mambo mengi sababu pia tunataka short cuts katika maisha. sioni issue kubwa hapa ya huyu dada kua mwathirika ipelekee kumharibia maisha yake kabisa maana kuna kaka asojua ukimwi ni nini anataka kuvuruga ndoa ili aonekane mwema.
 
Kwenye makanisa ya kiroho ndoa haifungwi Bila kupima ukimwi Kwanza kama wamekwepa wote wawili wanamatatizo
 
Kwa hali ndo maana tutatoa elimu kindagateni mpaka chuo kikuu bure aisee
 
Angekua mwanao ungemwambia kama mke sie au ungemchunia? fanya maamuzi sahihi okoa maisha ya mwenzio...
 
mkuu tupe Elimu zaidi kuhusu huu Ugonjwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…