KWELI Dagaa huwa na faida kubwa kwenye kuboresha Afya ya mifupa kuliko Samaki wakubwa

KWELI Dagaa huwa na faida kubwa kwenye kuboresha Afya ya mifupa kuliko Samaki wakubwa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mdau wa JamiiForums ametoa hoja yake kuwa watu wanaokula dagaa hupata faida kubwa zaidi kuliko wale wanaokula samaki wakubwa.

E4DE73B0-8148-4083-94F7-470DA3F5B5CA.jpeg

Amedai kuwa tofauti na samaki wakubwa, mtu anayekula dagaa anakula hadi mifupa yake yenye madini mengi ya calcium hivyo kuwafanya wawe na mifupa imara kuliko alaye samaki wakubwa, hasa kwa watoto ambao wanakua.

Amewashauri watu kutumia dagaa kwa wingi, ikiwezekana wawepo kwenye kila mlo.

Madai haya ni sahihi?
 
Tunachokijua
Dagaa na samaki hupatikana kwenye kundi moja la viumbe vyenye uti wa mgongo, maarufu zaidi kama vertebrates. Kwa pamoja, vitoweo hivi huwa na sifa nyingi za kufanana ambazo hutofautiana kidogo sana kulingana na mazingira, pia aina ya maji wanayopatikana.

Ili kulinganisha faida ya kipi ni bora kati ya dagaa na samaki, ni muhimu kuzingatia aina maalum ya dagaa na samaki inayozungumziwa kwa wakati huo.

Hata hivyo, kwa ujumla, samaki na dagaa ni vyanzo bora vya protini, asidi ya mafuta ya omega-3, vitamini na madini.

Faida kwenye mifupa.
Madini ya calcim huhifadhiwa kwenye Mifupa na meno ya binadamu zaidi ya 99%. Madini haya hupatikana yakiwa kwenye mfumo wa calcium hydroxyapatite (Ca10[PO4]6[OH]2).

Baadhi ya virutubisho hasa protini na mafuta ya asidi ya omega 3 hupatikana kwa wingi zaidi kwenye samaki kuliko dagaa. Kwa hivyo, kulingana na aina ya samaki, inawezekana ikawa ni bora kula dagaa kuliko samaki au ni bora kula samaki kuliko dagaa.

Hata hivyo, kwa mujibu wa USDA, Dagaa huwa na kiasi kikubwa zaidi cha madini ya calcium kuliko aina nyingi za Samaki. Madini hayo hupatikana kwa wingi kwenye mifupa ya dagaa ambao mlaji huitafuna moja kwa moja wakati wa kula, tofauti na ilivyo kwa aina nyingi za samaki ambazo huwa na mifupa mikubwa isiyoweza kutafunika kirahisi.

Kwa kufanya marejeo ya data za USDA kuhusu mgawanyiko wa virutubisho na madini yaliyomo kwenye vitoweo hivi, JamiiForums tumebaini kuwa dagaa huwa na kiasi kikubwa zaidi cha madini ya calcium ambayo huhusika kwenye kutengeneza mifupa ya mwili wa binadamu.

Pia, tumebaini kuwa dagaa huwa na faida nyingi zaidi kwenye kuboresha afya ya mifupa kuliko samaki wakubwa.

Hata hivyo, ni muhimu kujua kwanza aina ya virutubisho unavyohitaji kwani baadhi yake hupatikana kwa wingi zaidi kwenye samaki kuliko dagaa, mfano protini na asidi ya mafuta ya omega 3 ambayo ni muhumu kwa afya ya ubongo, ini na moyo.
Asante chief kwa elimu,
ni dagaa aina zote au dagaa wa aina fulani tu ndio wanafaida zaidi?
 
Back
Top Bottom