Dah, kweli tunatofautiana.......

Na mpenzi wako unaweza ukaongea chochote.
Baada ya dakika 3 za maongezi muhimu zinazofata mara nyingi ni pumba.
Pumba nazo muhimu kwenye mahusiano. Zinanogesha.
 
Kama ni demu wangu haina shida, mi nachonga naye tu hata masaa 24 ili mradi tunayoongea hayana ubaya wowote. Mi napenda mpira na demu wangu alikuwa hapendi kabisa lakini tukichanganya story anaanza kupenda. Unaweza kuongea na mwanaume mwenzio bado mkaongea pumba vilevile. Labda kama unayeongea naye sio demu wako au siyo mtu wa karibu unaweza ukajiuliza kidogo. Kuna vitu vingi vya kuongea na kama mwanaume bado unaweza kumwambia demu wako kuwa nguo flani ilimpendeza. Mbona ukitongoza unasifia hadi hereni bwana, itakuwa kumwambia demu wako vitu kama hivyo. Nadhani hakuna tatizo, ukiweza kuongea muda mrefu au muda mfupi, cha muhimu ni kuwa wote mnakuwa na furaha na mnaridhika. Kuna demu anaweza kuwa anapenda muongee sana, we ukijifanya hutaki kuongea sana, watakuja wanaoendana naye halafu, freeesh. Maisha ndo haya tunayoishi, so kama haumkeri mtu mwingine au jamii kwa ujumla, fanya tu unachojisikia.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…