Dah! Muacheni Diamond kidogo

Daudon

Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
63
Reaction score
87
Huyu Mange ni shida. Akiamua kutumia uwanja wake kushambulia mtu yani ni shida. Juzi hapa Kiba alipotoa wimbo wake watu (akiwepo yeye) waliona kama ajabu vile kwa Kiba kufikisha views 1m kwa saa 24 kupitia youtube. Leo Diamond kapata views hao hapo kwa muda huo lakini anainekana ni 'mwizi' wa views. Diamond hajasema kitu yeye anapost tu kazi zake.

Kabla ya hapo wakati wa mobeto kuwa na mimba hadi kujifungua kijana wetu alisakamwa sana na huyu dada, ambaye kwa namna nyingine namkubali tu. Kila mara alipost habari za Abdul na mwisho wa siku Abdul alikuja kuongea na kuwanyamzaisha kwa hayo.

Sasa nimeona tena kuhusu ndoa ya zamaradi mara Zari kahusishwa tena. Kwamba Zama ndiye strong woman kisa kafanya maamuzi ya kuolewa.

Leo mpinzani wa Abdul ambaye ni Kiba yuko vevo. Mange naye huyo. Anataka Diamond aende huko kushindana na Kiba...

Mange endelea na michango dada. Kama Diamond alikukosea msamehe tu na maisha yaendelee. Ni hayo kwa sasa maana nami usijenigeuzia kibao maana wewe huchelewi kugombama hata na kivuli

 
Naona wafuasi wake wanamuamini kama misukule, kila analosema kwao ndio na huyu dada kama angefungua kanisa angepiga ela nyingi ya sadaka kwani wafuasi wake WENGI wao ni wajinga ,kila kitu mange kasema yaani kinajifanya kinajua kumbe sometime kinawaingiza wenzake chaka. Mtu kama huyu kufanikiwa kazi, moyoni amejaa CHUKI na ndio maana mungu hawezi mbariki kwani mungu hukaa na kuwabariki wote wale ambao mioyo yao imejaa upendo. Ila sitoshangaa siku akija chambua mpira, kwani kimezoea kuropoka.
 
Ukipaa sana juu kila mtu anakuona kwa kuinua tu macho hivyo pia kwa wale wabaya wanapata target, huku chini mbanano ni mkubwa! Umchukiaye hata ukiinua macho humuoni maana mko kwenye ground moja, kiba bado haonekani, akianza kupaa kama Mondi basi atapigwa mawe nae.
 
kijana wanamuandama sana ila kitu kizuri hakati tamaa
 
Mastar wakubwa duniani wako VEVO..why Mondo..ujanjaujanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…