Dah! Warning Letter imemchanganya sana Eng Haizai Kamwelwe! Kwani hajajenga? Au bado anasomesha?

Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2017
Posts
3,373
Reaction score
6,795
Sikutegemea kama warning letter ingeweza kumchanganya kiasi hiki mwanasiasa mpendwa eng Haizai Kamwelwe..

Haya mambo yalitakiwa yamchanganye kijana anayeanza maisha, au mtu ambaye anasomesha na hajajenga.

Kwa uinjinia wake huo hata akioneshwa mlango wa kutokea kwani ataweza kukosa tenda za kujenga nyumba mitaa yote hii ya jiji ambayo ujenzi unaendelea kila kukicha?

Injinia, acha woga.. Chapa kazi.. Hayo mambo ni ya kawaida tu.

Maji ya moto yashapoa mzee wangu.
 
Kila binadamu huwa kuna wakati anakuwa na hofu labda huo ndio ulikuwa wakati wake!au ilikuwa ni plan ikae hivyo ili kutuliza maswali kwa jamii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujaelewa kwamba ukitumbuliwa huachiwi uishi kwa raha, ingekuwa hivyo wengi wasingeogopa kutumbuliwa.

Sasa hivi ukitumbuliwa unafuatiliwa, unakuwa blacklisted na unaweza hata kutafutiwa kesi ya kubambikiwa.

Kuna Mkuu wa Mkoa kajiuzulu, rais anamsakama kama hakuwa na haki ya kujiuzulu.

Na huyo kajiuzulu, hajatumbuliwa.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Nani huyo boss.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…