Mbunge Luhaga Mpina amesimamishwa kushiriki vikao kumi na tano vya Bunge, lakini mimi nitasimama upande wake daima. Mpina ni mtoa taarifa muhimu kuhusu jambo ambalo wengi hawalijui, na hivyo ingekuwa vyema Bunge likaunda Kamati ya kuchunguza ukweli wa jambo hili.
Je, inakuwaje Waziri Bashe anawapa kampuni ya vifaa vya ofisini jukumu la kuagiza sukari? Inakuwaje upungufu wa sukari unakuwa tani 30,000, lakini Waziri Bashe anaagiza sukari tani 410,000? Inakuwaje kampuni inasajiliwa mwezi mmoja baada ya kuanzishwa na kupewa kibali cha kuagiza sukari? Inakuwaje upungufu ni tani 30,000 lakini inaagizwa tani 410,000, na hivyo Serikali inapoteza kodi kwa hizo tani za ziada?
Haya yote yanahitaji uchunguzi wa Kamati ili kujua ukweli ndani yake. Mimi bado naamini kuwa Waziri Bashe ana makosa na ni vyema mteule wake amweke kando kwa sababu kuna sintofahamu nyingi kuhusu mambo aliyoyafanya. Usiwaone wananchi wamenyamaza; wengi tuko upande wa Mpina.
PIA SOMA
- Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15