Dakika 45 ndicho kipindi bora kwa sasa Tanzania

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Tukiacha ushabiki na ukanda usio na kichwa wala miguu kipindi cha ITV saa tatu usiku siku kila Juma tatu ndicho kipindi bora chenye kufundisha, kuelimisha na kutukutanisha na watu wenye weledi mbalimbali.

Nafuatilia kwa sasa na nimemuelewa sana ALI MUFURUKI sio siri tuna watu portential sana tatizo tu hatujui namna ya kuwatumia.
 
unaangalia kupitia kin'gamuzi gani
 
Umetumia vigezo gani kusema ni Bora?
1, Uwezo na umahiri wamtangazaji, Kilianza na Suleimani Semunyu akaja Sam Mahela sasa ni Deo Rweyunga

2,Mpangilio na mtiririko wa mada kimaana na kimaudhui

3, Watu wanaohojiwa ni waliomo ktk idara wanazozizungumzia na wanauzoefu mkubwa tu mfano mawaziri wafanyabiashara wakubwa nk Media nyingine kupata watu wao sijui hawawez au vipi mimi sijui

4, Muda uliowekwa, ni conviniete kwa kila mti yani jumatatu saa3 usiku

5, Media husika, huwezi ukaongelea serious media ukaacha kutaja ITV utakuwa biase..

Niendelee mkuu.?
 
Hapa ndio huwa siwaelewi watanzania,kwani kuna hadi ukanda katika kuvipenda vipindi vya television?

Ni kwamba Tanzania imefikia hatua hiyo?

Na hii ndio imekuwa tabia ya wanasiasa na baadhi ya viongozi kuwataka watu waweke mbali tofauti za kikanda,kikabila na kidini,hivi ni nani aliwaambia watanzania wanajitazama kwa makabila,kanda na dini zao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…