Daktari afichua vijana wengi wana tatizo la nguvu za kiume

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368



KUMEKUWA na ongezeko kubwa la vijana wanosumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume, likichangiwa kwa kiasi kikubwa na msongo wa mawazo, imefahamika. Hayo yamebainishwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa mkojo na jinsi ya kiume katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma, Dk Remigius Rugakingira alipokuwa akielezea huduma na tiba zinazotolewa katika kitengo hicho Urolojia, ikiwamo matatizo ya nguvu za kiume na uzazi wa akina baba.

Dk Rugakingira alisema idadi kubwa ya wagonjwa wanaoka katika hopitali hiyo wakiwa wanakabiliwa tatizo la nguvu za kiume ni vijana, ambao wengi wao tatizo hilo linachangiwa na msongo wa mawazo huku wazee ndio wakiongoza kuwa na matatizo yatokanayo na tezi dume. “Hali ya maisha, uchumi, mahusiano ya jamii na wenza wao, hivi ni sehemu inayomfanya kijana kuwa na stress (msongo wa mawazo) ambao umekuwa ukichangia sana tatizo la nguvu za kiume na uzazi kwa vijana,” alisema. Alisema mbali na kutoa tiba ya kibingwa kwa watu wenye matatizo ya nguvu za kiume na uzazi wa akina baba kwa kutoa dawa au kufanya upasuaji kulingana na ukubwa wa tatizo, pia wamekuwa wakitoa tiba ya ushauri hususan vijana ambao matatizo yao yametokana na msongo wa mawazo.

Dk Rugakingira alisema chanzo kingine kinachochangia tatizo la nguvu za kiume ni kisukari, uzito uliozidi, matumizi yasiyo sahihi ya dawa, tezi dume, bawasili (hemorhoids) na kutopata chakula bora. “Kuna haja sana ya kutilia mkazo suala la lishe, miaka ya nyuma watu tulifundishwa somo la sayansi kimu tangu shule ya msingi hili lilisaidia kutambua aina na vyakula ambavyo ni muhimu na husaidia katika kuondoa magonjwa mengi yakiwemo ya nguvu za kiume na uzazi wa akina baba,” alisema. Aidha, alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Watanzania wenye matatizo ya nguvu za kiume na uzazi wa akina baba kuka Hospitali ya Benjamin Mkapa ili kupatiwa matibabu ambayo yamekuwa yakitolewa kwa teknolojia ya kisasa.

“Mtanzania ambaye ana shida kwenye nguvu za kiume au uzazi wa akina baba hawatakiwi kuwa wanyonge au kutafuta suluhisho kwa njia zisizo sahihi na hatarishi, huduma hizo zinatolewa hospitalini hapa na wengi wametibiwa na kupona,” alisema. Kitengo cha Urolojia pia kimekuwa kikitoa huduma ya matibabu ya magonjwa mbalimbali ya mfumo wa mkojo na jinsia ya kina baba yakiwemo magonjwa ya tezi dume, magonjwa ya njia ya mfumo mkojo, kansa katika mfumo wa mkojo, uvimbe maji katika go, upasuaji kwenye kokwa za kiume, ngiri maji. Pia hopitali hiyo pia imekuwa ikitoa huduma kwa watoto ambao njia za kukojolea hazijakaa sehemu husika (hypospadias). Aidha, kuanzia mwaka huu, hospitali hiyo itaanza kutoa huduma ya kuvunja na kuyeyusha mawe kwenye njia ya mfumo mkojo (go, mirija ya go na kibofu) kutumia huduma ya kisasa ya mionzi.
 
Tuvute subira,Iko siku pia wataleta takwimu ya upungufu wa nguvu za kike
 
Kijana Wakiume Unakuwa Na Idi Nyingi Hadi Za Kike? Huku Si Kupungukiwa Na Nguvu Za Kiume Tu Bali Ni Kupungukiwa Akili Pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…