Daktari alifanya nikampoteza mchumba wangu Mercy

Me nimelipenda jibu..
Hiyo ni Bonge ya silaha ya kiume lazima limuume
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣Kha!Kweli hupendi ujinga....
 
Hii episode imekurejeshea heshima uliyoipoteza kwenye episodes zingine.
 
Dr hakumpenda Mercy,,alitaka tu kuonyesha ubabe
NAhisi kwa sababu wao walimfata kumwambia aachane na mercy..

Na hilo ni kosa kubwa sana Alilofanya DeMostAdmired kama Mwanaume..

Mwanaume yoyote ukimfata kumshurutisha kitu ambacho hajakifanya ni kama unamtilia Petroli kwenye Moto na kumwambia.."Lets Race" yaani walivyomfata siku ile ni kama Dr alikuwa anasikia "Are you ready for Ruuuumbbleeee"

Na ndo maana alifanya kila njia achape hiyo kitu na Nakuhakikishia kuwa akishachapaa mara kadhaa akiona kaishinda mecho anamtema
 
Yeeez zaaa
 
Dah tunashukuru sana kwa muda wako,stori inasisimua sana
 
Huyu dogo atakua alimfata Dr kibabe, kwamba achana na kumfatilia demu wangu, huwezi kumpata, demu ananizimia sana Mimi, utapoteza tu muda wako ila angeenda Kwa adabu. Akamwambia bro najua wewe una Hela na unaweza kufanya lolote Kwa Mercy ila mdogo wako nampenda Mercy na Nina mpango wa kumuoa, naomba niachie bro. Angemuelewa Kwan sisi wanaume ni waelewa sana hasa kama ndo unaanza tu kumfatilia demu Bado hujapiga. Naamini approach yake Kwa Dr haikua Nzuri na ndio maana Dr alipofanikiwa akaanza kumtumia sms za dharau maana alitaka kumuonesha dogo hakuna kinachoshindikana
 
Hivi wewe DeMostAdmired na huyo dakatari mnapata wapi nguvu ya kugombania mwanamke mmoja, yaan mimi ni huu uvivu wangu wa kutongoza wanawake, nianze kugombania mwanamke mmoja aisee naona kama ni kazi ngumu kupita maelezo.
Kutongoza tuu mwanamke nahic kama ni tiresome process, sembuse kugombania.

Kwanza nikiona tuu mwanamke ana mtu mwingine interest yote inapotea, pia nikiona mwanamke niliyokuwa nae ana interest na wanaume wengine interest huondoka(hapa nazungumzia ku-reply message za wanaume ambao anajua kabisa wanamtaka), sasa nyie wanang mkoje????

Ningekuwa wewe baada ya kupata ushahidi wa usaliti, ningeenda kwake kiroho safi tuu, ningechukua vitu vyangu vyote, ningehakikisha na yeye hajaacha kitu kwangu, then ningekata mawasiliano, sio kum-block wala sio kutopokea simu zake, ni kukaa tuu kimya, simpigii na sijibu text zake, akipiga napokea namsikiliza, akituma message sijibu, akiniuliza shida nn namjibu "Niko sawa".

Najua inauma lakini if a woman doesn't want to be what you want her to be, don't force or cry about it, just move on, yes it's going to hurt but that's life, life is not supposed to be easy, especially when dealing with emotions, kuna muda ndio utam-miss na uta tamani umpigie lakini utakapo fanya hivo utashusha dhamani yako, wanaume tuelewe kwamba mwanamke aliyekusaliti ukamsamehe hatakuona una upendo au mvumilivu atakuona mpumbavu na huna uanaume kwasababu mwanaume wa kweli hasamei usaliti, unapomsamehe au kumchekea au kumkalia kimya mwanamke aliyekusaliti ni kama vile unamwambia "Mimi sio mwanaume" na hio kitu naona wanaume wengi wanafanya.

Mwanamke aliekusaliti ukaachana nae pamoja na yeye kuomba msamaha hata kutoa machozi yote atabaki anakuheshimu milele, lakini mwanamke aliyekusaliti na ukamsamehe atabaki anakudharau milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…