Ndiyo Ile miosho ya chuo ilimzingua akajiona malkia...mwenzie alimuomba amzalie akakataa matokeo yake kaenda kuzalishwa na mume wa mtuUnajua zile akili za kichuochuo hiyo x-trail akipandishwa alikuwa anaona kama ya kwake vile
Ndio chanzo cha Hill jina?Hii inshu nilichelewa kuipitia ila imekuja kunitokea kwa kimchepuko changu nilichokuwa nakiamini sana,mpaka sasa naamin hakuna mwanamke ambae wajuba wakimtaka na akaruka
Kwanza nilishangaa kinabadili funicha za ndani haraka haraka tu nikaanza kupata wasi wasi
DR Mambo Jambo haya Kuna mwenzio kajitokeza hukuHapa ndo ulipotibiwa
View attachment 2917015
View attachment 2917016
Unaikumbuka Hii offisi unamkumbuka nani kati ya hao..View attachment 2917017
Binadamu Amepewa Uwezo Wa Kusahau Bila Hivyo Watu Wasingekuwa Na Furaha.
Huyo ndo Muhusika sasa Mimi naona mnanisingizia tuDR Mambo Jambo haya Kuna mwenzio kajitokeza huku
Ngoja mimi nitunge sasa maana yangu mimi sio halisia 🙂😃😄😄Dr achana na Hizo dawa,tunataka mwendekezo wa series baada ya Mercy kujifungua unampa Matunzo mtoto?au ndio anakula ugali wa Babu yake?
NashukuruNilichokiona mimi kwenye somo hili bwana Admired bado anampenda Mercy kutoka moyoni kikwazo ni mtoto tu kulingana na maandishi yake na pia nadhani amekutana na wasichana kadha wa kadha lkn wengi hawajafit kwenye vigezo vya jamaa ikiwemo huyo Marry yaani ilotokea emergence lkn hafit kwenye cretaria za msela
Sasa nini kitatokea mbeleni!!!?
Hapa kuna mambo wawili ambayo yataendelea kumtafuna jamaa mpk aje mwanamke wa vigezo vya Mercy na si suala la rahisi kufanikisha japo inawezekana akiwa mvumilivu
Pili jamaa akimuoa Mercy hakika mateso hayatakoma kwake labda Dr afe maana yeye ( dr ) yupo kwa ajili ya kumkomoa jamaa yetu na anajiona mshindi na hana mpango hata na huyo Mercy wa kumuoa hata mke wa pili
Tatu ,kama inawezekana mshauri Mercy aolewe na mtu mwingine kabisa asiyejua background ya nyie wawili ( dr na wewe) hiyo itamleta amani ya kudumu
Nne, kwa kuwa binti alijigeuza mwili wake kuwa chombo cha starehe na hakujali hasara aliyokuletea ikiwemo ya afya yako nadhani ni vzr uendelee kumpelekea moto pasipo kumshtua kama jinsi alivyopretend kuwa hamna kinachoendelea ili hali alijua nini anafanya pasipo kujali utaumia kiasi gani
Kwa wewe usijali dr anamla au hamli ,anawasiliana nae au laa ,anahudumia au vp wewe mpige pu...mbu tu siku akili ikimwijia ajue anatumika kote kote basi atachagua njia sahihi kwake
🤣🤣🤣Ila I wish angetokea Dr wa ukweli naye ashushe nondoHuyo ndo Muhusika sasa Mimi naona mnanisingizia tu
Nilitibiwa tabora hospital ya Kanda ya jeshi, pale asilimia 90 ni wajedaHapa ndo ulipotibiwa
View attachment 2917015
View attachment 2917016
Unaikumbuka Hii offisi unamkumbuka nani kati ya hao..View attachment 2917017
Huyo Dogo amedanganya kasoma First Year 2019/2020.. dogo kasoma pale 2017/2018DR Mambo Jambo haya Kuna mwenzio kajitokeza huku
Namaanisha alipong'olewa Jino mercy..Nilitibiwa tabora hospital ya Kanda ya jeshi, pale asilimia 90 ni wajeda
Mi ndo Muhusika ila Mercy alikuwa Mzuri acha tu na alikuwa na mvuto wa kushawishi..🤣🤣🤣Ila I wish angetokea Dr wa ukweli naye ashushe nondo
Makubwa 😳😳🥺🥺🥺🥺🥺Huyo Dogo amedanganya kasoma First Year 2019/2020.. dogo kasoma pale 2017/2018
Alisoma First Year 2017/2018
Na walikuja Hospitali
na Ilikuwa Ni Mazimbu Hospitali Kitengo cha Meno 😀😀😀
Na Dogo Alisoma BSc ED Chemistry and Biology
😅😅😅🤣🤣🤣Ila I wish angetokea Dr wa ukweli naye ashushe nondo
Acha kupotosha ummaMakubwa 😳😳🥺🥺🥺🥺🥺
Muongo haikuwa hospital hiyoNamaanisha alipong'olewa Jino mercy..
Safi sana mdogo wangu kwa uandishi wako mzuri,nimekufatilia tangu mwanzo mpaka mwisho na hii story sio ya kutunga maana hisia ulizoonesha kuelezea hio ni first love...na wengi tumeipitia hata kama hatujaeleza....ushauri wangu "Huyo mercy mwache abaki hivyo usije ukamwoa maana,,,,huyo doctor hataondoka kwenye maisha yake kwa kigezo cha uyo mtoto"""" pambania kombe na maisha mengine yatakujia kimafanikio kila la kheriTuendeleee.......
Hapa nikaona kabisa Mercy hakuwa na mapenz na Dokta ila shida ni tamaa za pesa na Dokta alikuwa hana mpango wa kumuoa Mercy ila alihitaji kunikomoa tu. Nilihisi vile baadae baada ya siku moja Dokta kunitumia ujumbe "dogo wanaume tushafanya yetu ole wake hiyo mimba mkaitoe".
Hii text alinitumia siku moja kabla ya Mercy kufanya jaribio la kuitoa ile mimba. Hii text sikumuonesha Mercy niliona kama ntamchanganya tu na Haina maana.
DOKTA ALIMTIA MERCY MIMBA KWA MAKUSUDI NA ALIMLAGHAI KWA PESA ZAKE, HII KITU MERCY MWENYEWE NDO ALINAMBIA.
Niliwaza kama Mercy alikuwa hampendi Dokta ni kwanini alikubali kufanya nae tena kavu siku zake za hatari. Sikupata majibu sahihi nikaamua kuipotezea tu japo niliishia kuamini kuwa pesa ndo ilimshawishi Mercy mpka kubeba mimba.
Swala la Mercy kwenda namimi kwao akanitambulishe sikulikubali niliona Mercy hajafikiria kwa kutuliza akili na pia binafsi sikuwa tayar kuoa mwanamke mwenye mtoto.
SIKU YA KUAGANA NA MERCY ILIKUWA NI MAJONZI SANA.
Nilimsindikiza stand akapanda bus kuelekea kwao. Mimi naye nilibaki kwanza pale town kuna mambo yangu nilikuwa nayafatilia.
Nilikaa kama mwezi hivi ukizingatia hata kodi yangu bado ilikuwa inasoma. Kipindi kile nipo bado pale town niliamua nimtafute Merry, Merry alikuwa tayar kashaondoka kwenda Field alienda mkoa wa dodoma. Nilipomaliza mishe zangu nikapak vitu vyangu nikaondoka nyumbani namimi.
Mawasiliano na Mercy yaliendelea ila upande wangu nilianza kuona Haina tena haja ya kumtafuta mara kwa mara ila yeye alikuwa ananitafuta sana ananisihi nimuoe hata kama bado sijajipanga yeye kwao pesa so shida sana. Aliahidi ataomba pesa ya mtaji tuanze kuzichanga mdogo mdogo ila mimi nikaona kabisa Mercy nikimuoa na tayari kazaa na Dokta nitakua nimejitia kitanzi na kujibuturia kistuli mwenyewe.
Matokeo ya semester ya mwsho yalitoka na mimi na Mercy sote tulifaulu vizur hakukuwa na mtu mwenye kimeo.
Japo nilikuwa bado naumia kumkosa Mercy lawama zangu zote nilizielekezea kwa Dokta na niliahidi kutokuja kumsamehe yule jamaa.
Ilikuwa mwez wa1 mwaka jana Mercy alijifungua mtoto wa kiume na anamuita Johnson, still Mercy ananisisitizia nimuoe lakini bado sioni kama kumuoa Mercy nitakuwa nimefanya jambo la msingi.
Mimi naye hali yangu ya kiafya ilichange ghafla nakumbuka ilikuwa mwez wa 12, 2022 hata graduation sikufanya, nilipatwa na kama kistroke flan yani upande wa kushoto haukuwa sawa. Nilishindwa kutembea, nilipoteza uwezo wa kuongea kwa takriban wiki Moja yani mdomo ulikuwa mzito sana ila nilikuwa natumia maandishi nilipokuwa nahitaji kuongea na mtu.
Nilipelekwa hospital nashukuru Mungu pamoja na madaktari walifanikisha kunipa huduma nikarudi katika hali yangu ya kawaida.
Nilitumia madawa tofaut tofaut ila kuna hiyo moja siwez isahau. Najua kuna wataalam wa afya humu wanaijua vizuri inaitwa "Aten" sijajua kama ndo jina linaishia hapo au linakirefu chake. Hii dawa bhna nakumbuka siku hiyo nilikuwa bado siwez kuongea mtaalam akaagiza ikachukuliwe hii dawa, ni tu vidonge tudogo sana kiumbo, niliambiwa nimeze kamoja tu kwa siku ila mziki wake hii dawa sio wa kitoto.
Hii dawa ukiitumia inakufanya upate ham ya kuongea, inakufanya ujihisi raha yani sinywi na sijawahi kutumia pombe lakini nature ya hii dawa inataka ifanane na tabia ya pombe. Nilikuwa naambiwa nimeze kimoja kwa siku lakini nilikuwa nataman nipige hata tutatu kwasababu yani vilikuwa vinanichangamsha kwanzia kichwani mpka sehem zingine za mwili.
Nilipona kabisa na mpka sasa niko poa.
Mercy naye anaendelea vizuri na mtoto wake na kila siku ananitafuta (hata asubuhi hii kashanitumia text) tunaongea na kuchat saana. Kila siku ananikumbusha kuhusu swala la ndoa na anasisitiza sana nimuoe kwani ananipenda lakini mimi bado sipo tayar kwasababu Mercy tayar anamtoto na sio mtoto tu ila mtoto ni wa Dokta mtu mwenye ROHO mbaya.
NIKIONA KUNA HAJA YA KULETA MREJESHO JUU YA MIMI NA MERCY BASI NITARUDI KUWAPA MREJESHO JUU YA NINI KINAENDELEA LAKINI MIMI BADO SIONI KAMA NINAWEZA KUMUOA MERCY.
Naomba kufunga Uzi wangu kwa kuwashukuru nyote na nawatakia kila lakheri katika safari yenu hapa duniani hasa katika ulimwengu wa mapenzi.
AHSANTENI 🫶🫶🫶.
Nashukuru sanaSafi sana mdogo wangu kwa uandishi wako mzuri,nimekufatilia tangu mwanzo mpaka mwisho na hii story sio ya kutunga maana hisia ulizoonesha kuelezea hio ni first love...na wengi tumeipitia hata kama hatujaeleza....ushauri wangu "Huyo mercy mwache abaki hivyo usije ukamwoa maana,,,,huyo doctor hataondoka kwenye maisha yake kwa kigezo cha uyo mtoto"""" pambania kombe na maisha mengine yatakujia kimafanikio kila la kheri