Daktari aliyekuwa akimtibu Maradona anachunguzwa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001

Waendesha mashtaka nchini Argentina wanamchunguza Daktari wa, Diego Maradona(60) kwa uwezekano wa kuua kufuatia kifo cha nyota huyo wa soka kilichotokea Novemba 26,2020.

Polisi Mjini Buenos Aires wameisaka nyumba na kliniki ya daktari huyo Leopoldo Luque huku wakijaribu kubaini iwapo ulikuwepo uzembe katika matibabu baada ya upasuaji aliofanyiwa Maradona.

Maradona alifariki dunia kutoka na shinikizo la damu nyumbani kwake ambako alikuwa akiendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji.

Dokta Luque bado hajashtakiwa na amekuwa akikana kufanya kosa lolote.

Maradona alifanyiwa upasuaji kwenye mshipa wa ubongo kutokana na kuganda kwa damu, uliofanikiwa mapema mwezi huu na alikuwa akipata matibabu kutokana na uraibu wa pombe.
 
Kashakufa waachane nae, hivi hawajui maradona angendelea kuwa hai ni fursa kwa dokta
 
Kwa hiyo wanataka kutuambia kuwa doctor kachangia kifo cha legend!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…