Daktari asema Nyama, maharage mekundu hatari kwa afya

sio mtu aache kula nyama kabisa ........lakini tupunguze na pia tufanye mazoezi.
 
waache porojo zao...........wanataka tukae kama yule jamaa wa India anayesema hajala kwa muda wa miaka 70!
 
kwetunikwetu lazima tukubali ukweli wa kuwa watanzania (hasa wenye viji pesa) hatuko healthy.

mtu anakula zake nyama choma za kufa mtu anashushia na beer zake kadhaa na siku nzima alikuwa amekaa ofisini. Asubuhi kuna wanaokunywa supu ya nyama pia ( kwa vile ana hela), mboga mboga hakumbuki kala lini, he is overweight kukaribia obese pengine na hajijui.

tunahitaji kubadili namna ya tunavyokula ....................
 

Lakini mkuu tukumbuke kula ni necessity na pia ni starehe..........! Labda niongee kibaniani 'Vipi dugu yangu veve.....hujui soma.....biguni hakuna kula vala kunywa bana'
 
kama ukimsikiliza Dr, Isaack Ndodi sithani kama utakula kitu chochote maana almost every thing kina madhara
 
Mimi nadhani kinachohitajika ni ku balance vyakula tunavyokula kwani vyote vina umuhimu mwilini. Mfano waweza punguza ulaji wa red meat kwa kula mara moja kwa mwezi n.k. Lakini sio kuacha kabisa aina ya chakula labda tu uwe una maagizo maalum ya kitaalam kutoka kwa madaktari na wataalam wengine wa afya.
 
Wamasai wanakunywa sana dawa mza asili, thats why huwezi sikia mmasai anaumwa gout

Wamasai, Wahadzabe etc wanakula nyama ya kuchoma miaka nenda rudi na bado hawalalamiki kuhusu gonjwa la gout. Tatizo linatokana na watu kutofanya mazoezi.
 
Ukianza fuatilia haya utaambiwa ata ulivyozaliwa ulizaliwa kimadhara!
Iyo msg kwa mtanzania anayeishi kwa dola moja kwa siku haingii akilini na ndio % kubwa ambao wanakula apatacho na mola huwatetea na wako fit mpaka leo.
Ila sisi tunaondekeza usasa ndo twaumia mara gout,BP,STROKE etc
Kama una uwezo unaweza avoid ivyo but if not kula ushibe!
 
Tujenge mazoea ya kula samaki hasa fresh fish.
 
Tumeona tafiti nyingi kuhusu nyama nyekundu ikihusushwa na kusababisha magonjwa mbalimbali na sababu za kisanyansi zimetolewa. Kwa upande wa tafiti kuhusu maharage hususani mekundu bado sijaona tafiti yeyote.

Je huyu Dokta ametoa maelezo ya kina kuhusu athari na magonjwa yanayoweza kutokea baada ya kutumia maharage mekundu? Je yana kiambata gani kinachopelekea kutokea kwa madhari hayo kutokana na matumizi ya maharage mekundu? Je huo utafiti wake umehakikishwa kisanyansi?
 
As long as niko kijana, siwezi kuwa na dietary restrictions restrictions coz bado niko very metabolically active. Ni vijana wenye shule ndogo tu wanaokuwa na dietary restrictions while they are metabolically active. Suala la kujizuia kula baadhi ya vyakula linasababishwa na factors like age ambapo physiological and metabolic rate hupungua. Pia altered metabolism nayo hupelekea dietary restrictions. Lakini kama wewe u kijana halafu mzima, dietary restrictions za nini?
 
Napenda sana spea za ng'ombe dume na Mbuzi dume...kitu lainiiiii kama yai la kuchemsha!
 
That being the case vijana waliopitia boarding wote wangekuwa na hayo matatizo bse maharage nod ilikuwa daily
Inategemea umeyala kwa muda gani na kumbuka pia na suala la mazoezi, mashuleni haina shida sana watu hufanya mazoezi, fikiria sasa anayekula vyakula hivyo ni mtu mzima na si mtu wa mazoezi, tuzingatie ushauri wa wataalamu wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…