Daktari ashtakiwa kuiba moyo wa marehemu

Abx

Senior Member
Joined
Oct 16, 2012
Posts
139
Reaction score
78
Mkuu wa zamani wa uchunguzi wa chanzo cha vifo nchini Kenya ameshtakiwa kosa la kuiba moyo kutoka kwenye maiti iliyokuwa inafanyiwa upasuaji.

Dkt. Moses Njue alikanusha shitaka hilo aliposomewa mashitaka yake katika Mahakama ya Hakimu Mkuu Nairobi ambapo alikuwa ameshitakiwa yeye na mwanae pamoja na msaidizi wake.

Walidaiwa kuiba moyo wa Timothy Mwandi Muumbo wakifanyia mwili wake upasuaji Juni 25, 2015 katika chumba cha kuhifadhia maiti cha 'Lee Funeral Home'.

Hakimu Mkuu Francis Andayi aliagiza watuhumiwa wengine wafike Mahakamani na kujibu mashitaka kabla ya kesi kuanza kusikilizwa Julai 3.

Dkt. Njue alikanusha pia shitaka jingine la kuuharibu moyo ili kuficha ushahidi, akifahamu kwamba ripoti ya uchunguzi wa maiti hiyo ingetumiwa kwenye kesi iliyokuwepo Mahakamani.
 
Yaani muogope mwanadamu kuliko mnyama....Duh!! inatisha ...Na hawa ndio wasomi...
 
Yaani muogope mwanadamu kuliko mnyama....Duh!! inatisha ...Na hawa ndio wasomi...
Moyo wa maiti tu... sasa hapo inatisha nini??
Mbona unakuza mambo kama vile kaua yeye
 
Moyo wa maiti tu... sasa hapo inatisha nini??
Mbona unakuza mambo kama vile kaua yeye


The dead man was not an organ donor...So the dead mans remains in terms of law were violated and stolen...It is actually a crime to steal body organs from a human dead or alive...If the deceased has not given consent to mutilation of his remains it is unethical...But hey welcome to Africa...(My Swahili does not meet JF standards..easier to convey my thoughts in English..sorry)
 
Biashara ya viungo vya marehemu ni biashara kubwa na ya siri sana
 
Mkuu wa zamani wa uchunguzi wa chanzo cha vifo nchini Kenya ashtakiwa kwa kosa la kuiba moyo wa maiti iliyokuwa inafanywa upasuaji....

Chanzo: TANZANIA DAIMA
 

Attachments

  • IMG_20180517_080754.jpg
    165.4 KB · Views: 48
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…