Dokta kafika Kama kawaida kwa mpenz wake misheli, kaambiwa na mpenz wake akamwandalie kinywaji jikoni. Dokta anafika jikoni, anamimina juice kwenye glass kisha anavuta sumu yake mfukoni na kumiminia kwenye glass. Maaskali kule stoo wanamwona na kumvamia pale pale.
Dokta anatamahaki, maaskali Hawa hapa, wanamwambia uko chini ya ulinzi, unatuhumiwa kwa kumpa sumu mpenz wako, dokta anauliza sumu ipi, maaskali wanamwambia angalia juu ya friji, tuliweka camera yetu ya Siri tumekunasa.
Dokta anajitetea ile haikua sumu alikua anamuwekea virutubisho mkewe ambae Ni mjamzito. Maaskali wanampiga pingu na kuondoka nae.
Walipofika polisi, misheli. Anaitwa ili kuandika maelezo na kufungua kesi, Kisha maaskali wanaenda mahakamani kuomba search warrant ili wakamkague nyumbani kwake na kila kitu chake.
Walipoenda nyumbani kwake, wakakagua computer Yake, wakagundua email alizokua akiwasiliana na ex wake kumweleza jinsi gani hakua na mipango na misheli,kwanz mimba ile iliingia bahati mbaya na alipanga kuitoa.
Na kwenye maelezo yao, ex wake (nesi mapepe) anakazia kua hawez kudate na dokta kwa uhuru mpk ajiridhishe ile mimba ya misheli imetoka kabisa, yeye ndio mwanamke pekee anaepaswa kumzalia watoto. Dokta anasisitiza bado anaendeleza juhudi.
Walimkagua pia kwenye droo ya dressing table yake wakakuta bahasha ya kifungashio chenye lebo ya cytotec,na walipomkagua kwenye buti la gari , zikakutwa Chupa tano za unga wa cytotec na Moja iko nusu.
Dokta Alipoulizwa khs nesi mapepe, wamekuta kwenye simu yake ana mahusiano mengine ya Siri, akakiri kweli ana Mahusiano ya Siri ila hayahusiani na kumpa misheli Sumu ya kutolea mimba,yule Ni Mchepuko TU, anaomba maaskali wamtunzie iyo siri.
Walipomkazia khs email zilizokua kwenye computer yake nyumban wakiongelea kumtoa mimba misheli, dokta akakaa kimya.
Alipoulizwa khs cytotec kukutwa kwny buti la gari lake, akajitetea ana wagonjwa wa nje wanaumwa vidonda vya tumbo,uwa anawapelekea dawa Mara kwa Mara. Alipoulizwa majina Yao wakajiridhishe, akajitetea kua kiapo chake kinamzuia kutoa Siri za wagonjwa wake.
Maaskali wakaona mbali na ushahidi waliokua nao, mahakamani watahitaji shahidi wa kuthibitisha. Basi wakaenda kumuarrest nesi mapepe na kumwonesha email zote alizokua anachat na dokta. Na wakamwambia asipotoa ushirikiano Basi nae atajumuishwa na dokta kwenye mashtaka ya jaribio la kuua kwa sumu kwa kukusudia.
Nesi mapepe akakiri atasema ukweli wote Aya mambo yasifike mbali ataharibikiwa kazi. Maaskali wakamsihi afunguke uku wakaanza kumrekodi kisirisiri. Nesi akaanza kumkaanga dokta.....
**********************