Daktari: "Local Booster" (supu ya pweza, karanga mbichi, muhogo mbichi) Hazisaidii Urijali

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
ULAJI wa supu ya pweza, karanga mbichi, muhogo mbichi, mbata kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume kumeelezwa kuwa ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita kwa kuwa haina uhusiano kati ya urijali wa mwanaume na virutubisho vinavyotolewa na vyakula hivyo.

Kauli hiyo imetolewa na Dk Cuthbert Maendaenda wakati akitoa mada yake katika semina ya wahariri iliyofanyika mkoani Morogoro iliyojadili nafasi ya wanaume katika kuleta mabadiliko katika jamii juu ya afya ya uzazi na ujinsia.

Dk Maendaenda ambaye alikuwa akijibu maswali pia kuhusiana na dhana hiyo iliyozoeleka kuhusu nguvu ya supu ya pweza, alisema ipo haja ya wanaume kuangalia sababu za kudorora kwa uwezo wao na kufanya marekebisho badala ya kudhani kwamba kuna dawa kutoka katika vyakula hivyo.

Miji mingi nchini kwa sasa nyakati za jioni kuna supu ya pweza na mauzo ya karanga mbichi ambao wauzaji wamekuwa wakinadi kama msaada wa kurejesha heshima katika ndoa.

Alisema ufanyaji mapenzi unaathirika na vitu vingi na jamii lazima kuangalia ukweli huo ili kuwa na watu wanaojiamini katika mapenzi na wale ambao wanamatatizio kupata ushaudi wa kidaktari.

Chanzo: Michuzi Blog

 
Hili wala sishangai.

Jamii yetu inapenda sana kuamini amini mambo bila hata kujishughulisha na kufanya utafiti ili kubaini ukweli ni upi na uongo ni upi.
 
Hahahaaaa.... Wajuzi zaidi watakuja.
Nijuavyo mm vyakula ivyo vinaongeza protein na mafuta mwilini hivyo kuuamsha mwili kuzalisha mbegu za kiume na sio kuongeza nguvu.
Yatupasa kujiamini daima.
 
Ngoja wazinzi waje watakupinga utadhan walifanya utafiti..
 
Mchuzi blog Naona sasa kaishiwa point za kuandika ameaza kushabikia mambo ya kijinga kijinga.
 
huyo dr ni mgonjwa wa ebola kabisaaa yan navyo kamua pweza jion mixer na karanga mbichi uwa nakaaa nazo ofisini tena kabla cjafika maskan nina chimbo langu moja ilala nagonga maziwa ya ngamia. usiku nasimamia shoo adi najiona kero mbali ya hapo nikichepuka ndo uwa kama simba napingana wazi wazi na huyo dr
 
huyo dr ni mgonjwa wa ebola kabisaaa yan navyo kamua pweza jion mixer na karanga mbichi uwa nakaaa nazo ofisini tena kabla cjafika maskan nina chimbo langu moja ilala nagonga maziwa ya ngamia. usiku nasimamia shoo adi najiona kero mbali ya hapo nikichepuka ndo uwa kama simba napingana wazi wazi na huyo dr
 
  • Noted maziwa ya ngamia,
  • dola ngapi haya! Bila shaka yanakuwa imported from UAE
 
Mara nyingi nimekuwa nikiwacheka sana marafiki zangu wanapokuwa wanahangaika kutafuta karanga mbichi.
 
Daktari asema ulaji wa Pweza,karanga mbichi,muhogo mbichi,mbata kwa madai vinaongeza urijali kwa wanaume ni dhana potofu Chanzo:Habari leo
 
Ukweli mtupu..

Watu hawajui swala la sex linaanzia kwenye mind set kwanza...
 
Mchuzi blog Naona sasa kaishiwa point za kuandika ameaza kushabikia mambo ya kijinga kijinga.


Anajifanya yuko neutral kwa sasa kwani anajuwa mwakani CCM itakufa tu na hatakuwa na mtu wa kumbeba ili aendelee kula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…