Daktari: Matumizi ya Dawa za P2 huchangia mimba kutunga nje ya uzazi

Daktari: Matumizi ya Dawa za P2 huchangia mimba kutunga nje ya uzazi

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
1645530009189.png

Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake wa jijini Dar es Salaam, Godfrey Chale amewashauri wanawake wanaotumia vidonge vya kuzuia mimba maarufu kama P2 kuacha kufanya hivyo ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapata.

“Utafiti uliofanywa nchini Ghana mwaka 2003 ulionyesha kuwa matumizi ya vidonge vya P2 yamekuwa yakisababisha mimba kutungwa nje ya kizazi.

“Sijafanya utafiti kwa hapa Tanzania lakini nimeshapata kesi moja ya aina hiyo, kuna mama mmoja alikuwa na tatizo kama hilo (mimba kutunga nje ya kizazi), ikabidi nimuulize kabla alikuwa akitumia njia gani za uzazi wa mpango, akanieleza alikuwa akitumia P2.

“Mwanzoni wakati tunasoma (udaktari) tulielezwa matumizi ya kitanzi yanaweza kuchangia kuharibu mirija ya uzazi.

“Unakuta unapotumia matumizi ya kitanzi inachangia kuharibu mirija, mimba inapotungwa inashindwa kusafiri kwenye njia za uzazi.

“Katika huo utafiti wa 2003 huko Ghana ulionyesha kuwa wengi waliotumia P2 mirija yao ya uzazi iliharibika.

“P2 unatakiwa utumie mara tu unapofanya tendo na kuhisi kuwa kuna uezekano kuwa umepata mimba. Wanasema ni ndani ya saa 72 lakini unatakiwa utumie muda mfupi baada ya tendo.

“Sasa mwingine unakuta anatumia kabla ya tendo au mwingine anatumia siku moja baadaye, hivyo yai linapotoka P2 inakuwa haisaidii, matokeo yake ile dawa inaharibu mirija ya uzazi."

PIA SOMA
- Story of Change - Madhara ya P2 (njia 15 bora za kuzuia mimba/uzazi wa mpango)



Chanzo: Global TV Online
 
Back
Top Bottom