Benokolongokonongose
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 213
- 52
Habari zenu wakuu katika afya! Rafiki yangu amekuwa na shida ya kutopata mtoto yapata miaka miwili tangu andoeke(afunge ndoa). Alivyoenda kwa daktari akampima na akasema hana tatizo lolote isipokuwa nguo anazovaa zimemsababishia akose mtoto. Nguo hizi ni: Skin tights(vibana ngozi),suruali nk. Hoja ya daktari ni kuwa sehemu za siri hazihitaji kupata joto kali au kubanwa. Ni kama nimeachwa kwenye mataa. Kama ukweli ni huu si inafaa kuongezwa kwenye vyanzo vya uzazi wa mpango? Nawasilisha. Wenu Benokolongokonongose.