KERO Daladala Dodoma zinarubuni abiria kuhusu ruti na kutelekeza abiria

KERO Daladala Dodoma zinarubuni abiria kuhusu ruti na kutelekeza abiria

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Leo asubuhi eneo la Nyerere square baada ya konda na dereva kutudanganya kuwa watapitia General Hospital. Huyo dada hapo pembeni na kaka wagonjwa, mimi nilikuwa naelekea Majengo na konda akaanza kunitishia kunipiga na dereva nae akaanza kuwa mkali.

Baada ya kuongea na dereva wa gari tulilofaulishwa akasema haya nanukuu "Kiukweli utaratibu wa kuishia square ni wa kwetu sisi siyo wa Serikali husika, tuliamua kufanya hivyo ili kukwepa lawama kwa abiria ambao wanashuka vituo ambavyo tukifuata utaratibu wa Serikali hatutapita vituo hivyo" mwisho wa kunukuu.

Naomba Serikali itoe utaratibu haraka iwezekanavyo na ikiwezekana wahusika wa gari hii wawe mfano ineniuma sana kuwadanganya wagonjwa kwamba watapita hospitali halafu na kuanza kuwafaulisha.

Kosa jingine gari imeandikwa Nkuhungu St Gemma ila imeenda Mipango kufuata nini?

Picha hizi ni screenshot za video. Namba hizo ni za gari husika na huyo mwenye shati la draft ni konda

d11.png
d22.png
 
Inaonekana ni mgeni Dodoma ruti ya st gema gar inapita mipango na inasimama kabisa.Hyo kushuka General hospital ni madhaifu ya LATRA wenyew kulazimisha stendi ya machinga ili kuchangamsha soko gari ya nkuhungu ikiishia machinga abiria mjini wataendaje,hvo hvo kwa mipango waoneeni huruma na hao dala dala wanaonekanaga wao ndo wanamakosa mda wote
 
Sema mimi namsapoti huyu jamaa shida hawa makondakta ni waongo mtu ukiwa unapanda wanakubali kabisa tunapitia sehem flani halaf ghafla unashangaa mnashushwa njiani

Back
Top Bottom