Daladala wanakera sana kuweka mafuta katikati ya safari hasa ukiwa unataka kuwahi

Daladala wanakera sana kuweka mafuta katikati ya safari hasa ukiwa unataka kuwahi

Ricky Blair

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
463
Reaction score
1,009
Hakuna kitu nisichokipenda kama nikipanda daladala, boda au bajaji especially when kuna foleni na unataka kuwahi wao wanaingia sheri kujaza mafuta.

Hivi wanashindwa kuweka full tank na kujaza kila wanapomaliza trip kuliko kujaza katikati?
 
Kazi ya kuendesha daladala ni kama kucheza kamali. muda wowote unaweza nyang'anywa gari kwa visingizio mbalimbali ikiwa ni pamoja kesi za polisi. Sasa dereva ukijaza full tank itakula kwako hutabakiwa na senti mfukoni.
 
Kwani full tank inaisha kila wakimaliza trip 🤓🤓🌄🌄🙌
 
😂😂😂 waweke full tank wakati muda wowote gari/bodaboda inaweza kupelekwa kituoni?
 
Jamii Forum wote si mna magari , au lako uliliacha nyumbani mkuu !!
Kwani huwezi kupanda daladala Ukiwa na gari, Mimi napanda daladala sana tu. Huku pickup yangu nikiiacha tu

Ni wife tu baada ya kununua gari hajawahi kugusa daladala
 
Kwani huwezi kupanda daladala Ukiwa na gari, Mimi napanda daladala sana tu. Huku pickup yangu nikiiacha tu

Ni wife tu baada ya kununua gari hajawahi kugusa daladala
Shemeji hataki joto la kwenye daladala.
 
Na ni hatari kweli kwa gari la abiria kujaza mafuta likiwa na abiria ndani.

BTW:Vituo vingi vina matangazo kabisa yakitaka magari yazimwe wakati wa kujaza mafuta pamoja na mambo ya simu na sigara.

Je ni wangapi wanazima vyombo pale?
 
Sio hivyo tuu, utakuka daladala zimekaa kwenye foleni halafu muda wa kupakia abilia umefika, abiria mmesubiriana zaidi ya nusu saa mmejaa mnapoanza kuondoka kama mita 500 mbele linaingia kituo cha mafuta kujaza!!!

daa yaani akili za hawa watu wanazijua wenyewe!
 
Back
Top Bottom