A
Anonymous
Guest
Mimi ni Mkazi wa Arusha, nimekuwa Mdau wa muda mrefu wa platform yetu hii ya JamiiForums kwa muda mrefu, kero yangu mimi ni kuhusu Daladala kukatisha ruti na kuongeza nauli kinyume cha Sheria.
Huku Arusha na vitongoji vyake tuna changamoto ya usafiri hasa ikifika mida ya Saa moja usiku na kuendelea, vyombo vya usafiri hasa hizi ambazo kwa Dar mnaziida Daladala, wenzetu hawa wanakatisha ruti na wengi wanaongeza nauli zaidi ya ile ya halali.
Ombi langu mamlaka husika washughulikie hiyo kero na pia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) waweke utaratibu kuwe na tiketI kwenye hizi daladala, kwani najiuliza wao hawaoni hiki kinachoendelea au wanaona na wameamua kuwa kimya watuache tunateseka?