The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Kuna daladala huwa zinazingua sana. Yaani unaenda mahali lakini hawakufikishi kama inavyopaswa. Kwa mfano, unaweza kuwa unaenda mahali, lakini wakiona mmebaki watu watano ndani ya gari wanageukia mbali na kituo, au wakati mwingine wanakufaulisha kwenye gari lingine lililojaa na nafasi ya kukaa unakosa.
Imagine unajikuta umesimama wakati uliwahi mapema kituoni ili upate siti ya kukaa. Umetoka home umeng'arisha kiatu fresh ili ufike ofisini ukiwa vizuri then mtu anakutembeza kwenye vumbi unatokwa na jasho. Ukifika unanukia ubeberu fulani hivi unaanza kukwepa kukumbatiana na watu wazuri.
Ubaya ni kwamba unashitukizwa tu kuwa "Abiria, tumefika mwisho!" then kondakta anakuchekea tu kana kwamba upo tayari kushiriki naye ufedhuli huo.
Kuna wakati bajeti ya boda ni buku tu ila daladala akikushusha mbali na kituo gharama inaweza kufika buku-jero au mbili kabisa. Inakera!
Daladala za Mbezi-Kawe ziache ujinga huu. Kuna daladala za ruti hii huwa ni mwiko kwao kuingia stendi. Wanageukia mita kama 200 hivi kabla ya kufika kituoni ili wasipange foleni. Huu ni ukatili. Nauli zetu zinakuwa hazijaisha. Hapohapo wanapokuacha, ukigeuza na gari hadi kituoni wakati wa jioni wanakuchaji jero.
Sema nini, tusake hela tununue magari, Wakuu.
#SogaZaPedestrian