Dalali ndiye anayechelewesha biashara

Dalali ndiye anayechelewesha biashara

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara - 52:
Kama utafuatilia kwa undani utagundua kuwa biashara nyingi za upangishaji na mauzo ya mali mbalimbali kama vile viwanja, nyumba, mapagala, mashamba, vyumba vya kupanga, mazao, magari, visima vya mafuta, n.k, zinakuwa ngumu kuuzika au kupangishika kwa haraka. Wanaochelewesha biashara ni madalali, na sio wateja.

Kwa mfano:
Unauza nyumba yako kwa Tshs 50mil, lakini dalali uliyempa kazi anamtafuta mteja wa Tshs 100mil ili yeye apate baki la Tshs 50mil (nusu kwa nusu).

Hivyo pasipo wewe kujua dalali wako anaweza kuwakataa wateja ambao watafika na Tshs 60mil, 70mil, 80mil, au 90mil. Kwahiyo biashara yako inakuwa ngumu sana kuuzika au kupangishika kwasababu ya dalali, pengine ulikuwa unataka pesa ya haraka.

Njia za kufanya:
Ukimpa Dalali kazi ya kuuza mali yako (kiwanja, nyumba, pagala, shamba, gari, n.k) ukiona biashara yako inachukua muda mrefu kuuzika, unashauriwa kuwa mjanja sana. Ni ujanja wa kumzunguka dalali wako ili ufanikiwe kuuza mali yako haraka, hakikisha unawapeleleza (unawafahamu) wateja ambao wanashindwana na dalali wako.

Ukiwafahamu wateja walioshindwana na dalali wako watafute ukae nao chemba, itakusaidia kuuza mali yako kwa haraka sana; pia utagundua kuwa biashara yako ilikuwa inakwamishwa na dalali wako. Hivyo mfanye dalali wako kuwa chambo.

Right Marker
Dar es salaam.
 
Jamaa umeandika uharo mtupu, kama hutaki dalali tafuta mwenyewe wateja au tafuta mali mwenyewe zunguka bila dalali,
Pia kwa ushauri uuzaji wa nyumba viwanja, na vitu kama hivyo elewana na dalali kumlipa asilimia sio auze juu, kama unauza kitu labda 10M elewana na dalali kama ni 10% au 5% au 3% sio kumwambia dalali mimi nataka 10M iingie kwenye account, unadhani dalali ataanza kutangaza kwa 10M?
 
Madalali na wingers wanaharibu deals nyingi sana.
 
Wanatamaa MNO!!
Watakuja kuvamia uzi hapa.
Mm ua natangaza mali yangu mm mwenyewe bila wao na bznes inafanyika vzr tu.
Na hata nikitafuta mwendo n kutafuta bila Dalali pia napata bila shida.
All the best
 
Back
Top Bottom